Ibraah Amsifu Anjella, Amtaja Msanii wa Kike Mwenye Bidii

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Ibraah anayekuwa kwa kasi sanaa kutokea Konde Music Worlwide amejitokeza na kumsifia mwenzake Anjella ambaye pia amesainiwa lebo moja na yeye. Ibraah na Anjella walichipuka kutokea Konde Worldwide na kupata umaarafu kwa kasi mno.

Muziki zao nzuri ziliwafanya kupendwa na wengi na kufikia sasa wapo miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa sana katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Soma Pia: Anjella Ashukuru Konde Music Worldwide Kwa Kumkuza Kimuziki

Anjella hivi karibu alikuwa gumzo mtandaoni baada ya kuzawadiwa gari na Harmonize ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Konde Worldwide. Mashabiki wengi walijitokeza kumpa hongera. Miongoni mwa wale waliompongeeza ni mwenzake Ibraah amabaye alimsifia kwa kusema kuwa Anjella alikuwa msanii wa kike mwenye bidii sana.

Aliendelea kwa kumwombea mema kwa Mungu. Ibraah alikamilisha taaarifa yake kwa kumfahamisha Anjella kuwa wanachama wote wa Konde Worldwide Music wanampenda sana.

Soma Pia: Anjella Afichua Wasanii Atakaowashirikisha Kwenye ‘Nobody’ Remix

"Ni binti wa kike mpambanaji sana Mungu azidi kukufanyia wepesi we love you Queen @anjella_tz," ujumbe wa Ibraah ulisomeka.

Licha ya kuwa kwenye tasnia ya mzuki kwa muda mfupi sana, Anjella tayari amepanda ngazi na kulinganishwa na wasanii wa kike wenye uzoefu mkubwa sana kama vile Nandy na Zuchu. Licha ya kuibuka kwa tuhuma mtandaoni kuwa kuna uhasama baina ya Anjella na Zuchu kutokana na tofauti za wakubwa wao Harmonize na Diamond, Anjella amejenga mwonekano wa mtu pole asiyependa kashfa wala kiki.

Leave your comment