Nyimbo Mpya: K2ga Aachia EP Yake ‘Safari’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Kings Music K2ga ameachia EP yake ya kwanza kabisa tangu aanze muziki aliyoipa jina la ‘Safari’.

EP ya ‘Safari’ imesheheni ngoma tatu ambazo ni ‘Ni Wewe’, ‘Danga’ pamoja na ‘Goma’. Kwenye ngoma hizo zote hizo, K2ga hajashirikisha msanii yeyote bali ameimba mwenyewe.

Soma Pia: Video ya ‘Zai’ ya Maua Sama Kuwania Tuzo Uholanzi

 EP hii imetayarishwa na watayarishaji wa muziki tofauti tofauti kama Debee na Yogo Beats ambao wametengeneza ‘Ni wewe’ pamoja na ngoma ya ‘Goma’ huku Swabri Made It akiwa ametayarisha ngoma ya ‘Danga’.

EP ya ‘Safari’ inakuja mwaka mmoja tangu K2ga aachie ngoma yake ya mwisho ya kuitwa Lisambela ambayo nayo ilifanya vizuri sana.

‘Ni wewe’ ndio ngoma inayofungua EP hii na kwenye wimbo huu K2ga anatoa sifa kedekede kwa mwandani wake ambaye anampa raha za kutosha.

Kwenye ngoma ya ‘Danga’, K2ga ana mawaidha mazito kwa mwanadada ambaye ana tabia ya kutembea  na wanaume tofauti tofauti ili aweze kupata pesa. K2ga anatumia mdundo mujarab uliotayarishwa na Swabri kufikisha ujumbe kuwa ‘kudanga’ siyo tabia inayofaa.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Ujio wa ‘Only One King’ Tour

‘Goma’ ni ngoma ambayo K2ga anatumia lugha ya picha na kuelezea namna ambavyo anapendwa na mpenzi wake na bila shaka ngoma hii ambayo imetayarishwa na Debee na Yogo Beats itafanya vizuri sana kwenye mitaa na sehemu mbalimbali za kustarehe.

https://www.youtube.com/watch?v=6IPxMV2X4jA

Leave your comment