Dully Sykes Ajibu Madai ya Kutumiwa Katika Vita Dhidi ya Harmonize

[Picha: Muziki TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkongwe katika muziki wa bongo Dully Sykes hatimaye amejibu madai kuwa alitumika katika vita dhidi ya msanii mwenzake Harmonize.

Hapo awali, msanii nyota Harmonize alitikisa tasnia ya muziki wa Tanzania baada ya kufichua masaibu ambayo amepitia na jinsi wapinzani wake wanampiga vita na kujaribu kumshusha kimuziki.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Kwa Upana Sababu ya Mgogoro Baina Yake na WCB

Harmonize katika mahojiano aliyoyafanya alidai kuwa baadhi ya waliokuwa marafiki zake kwenye muziki kama vile Dully Sykes walitumika dhidi yake. Jeshi, kama anavyofahamika kimuziki, alidai kuwa Dully Sykes alimshtaki kwenye baraza la COSOTA kwa madai ya kutumia mdundo wake bila idhini.

Harmonize alisema kuwa madai hayo hayakuwa na msingi na Dully Sykes alitaka tu kumpaka tope ili apendeze mahasimu wake. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni na Clouds FM, Dully Sykes amejibu madai hayo ya Harmonize.

Staa huyo muziki aliapa kuwa hajawahi tumika na mtu yeyote. Pia alisema kuwa amemsamehea Harmonize kwa kutumia mdundo wa wimbo wake kwenye tangazo alilolipwa.

Soma Pia: Diamond, Zuchu na Nandy Wabwagwa Kwenye Tuzo za AFRIMA

"Ningependa kuambia watanzania kwamba sijawahi kutumwa, sijawahi kuwa mtumwa na sitokuja kuwa mtumwa mpaka nakufa wa mtu yeyote. Hao wanaodhania mimi wananituma, hawawezi kunituma. Ni sasa wananitukanisha, wananidharawisha, wananiweka kwenye kundi la wanafiki, wananiweka kwenye kundi la watu ambao sijui niseme nini. Yeye ameamua kuongea alichokuwa amefikiria kuongea," Dully Sykes alijitetea.

Hapo awali, Dully Sykes na Harmonize walikua na ukaribu mno na wakashirikiana katika ngoma kadhaa ambazo zilifanya vizuri sana.

Leave your comment