K2ga Atangaza Ujio Wa EP Yake Mpya ‘Safari’

[Picha: Mwanaspoti]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Kings Music K2ga ametangaza kuachia EP yake mpya aliyoipa jina la ‘Safari’.

K2ga ametangaza kuwa atatoa EP hio ijumaa ya tarehe 26 Novemba mwaka 2021. EP hiyo itakuwa ni ya kwanza kutoka kwake tangu aanze muziki.

Soma Pia: K2ga Aelezea Sababu ya Ukimya wa Kings Music

"Maisha ni Safari yenye milima na mabonde ya kupanda na kushuka na sehemu ya fumbo gumu sana. Changamoto za kwenye safari ya maisha ni msafiri pekee azijuae ndio maana waswahili wameibuka na msemo "Msafiri Kafiri". Kwa hiyo kamwe usimuhukumu mtu yeyote wala kumlaumu katika safari sababu huwezi kufahamu anayoyapitia mwingine," aliandika K2ga.

Mpaka sasa, K2ga bado hajathibitisha idadi ya ngoma itakayounda EP au ni wasanii gani watakaoshirikishwa kwenye kazi hiyo.

Soma Pia: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Addiction’ Akimshirikisha Harmonize

Mara ya mwisho kwa K2ga kuachia ngoma yake binafsi ilikuwa Septemba mwaka jana alipoachia ‘Lisambela’ ngoma ambayo ilifanya vizuri nchini Tanzania. Tangu hapo amekuwa akishiriki kwenye ngoma tofauti tofauti za King's Music ikiwemo ngoma ya ‘Ndombolo’ ambayo alifanya na Abdu Kiba, Alikiba na Tommy Flavour.

Wasanii wengi kutokea Bongo wameonekana kuwa na mwamko wa kuachia EP kwa mwaka huu. Kando na K2ga, wasanii wengine kama Quick Rocka, Mwasiti, Lavalava, Kayumba, Mac Voice, Rayvanny, Nandy na Hanstone nao wameachia EP zao.

Leave your comment