MB Dogg Asimulia Masaibu Aliyopitia Katika Muziki
23 November 2021
[Picha: MB Dogg Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mmoja wa wasanii wakongwe zaidi kwenye tasnia ya muziki wa bongo MB Dogg amesimulia masaibu ambayo ameyapitia kwenye muziki na sababu kuu ya nyota yake kufifia ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.
MB Dogg kwa miaka za hapo nyuma katika enzi ya zamani ya bongo alikuwa mmoja wa wasanii ambao walivuma mno. Staa huyo katika enzi zile alivuma kupitia ngoma kama vile 'Si Uliniambia', 'Natamani', 'Ina Maana' na nyinginezo nyingi.
Soma Pia: MB Dogg Aeleza Changamoto Anazopitia Katika Harakati za Kurejea kwa Muziki
Ila kadri muda ulivyosonga ndivyo nyota yake ilionekana kufifia kwenye muziki. Kupitia taarifa ndefu ambayo amechapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, MB Dogg amefunguka kuhusu mazito ambayo yaliathiri vibaya muziki wake.
Kwa mujibu wa MB Dogg, mambo yalianza kumwendea mrama mwaka wa 2007 baada ya kufanya uamuzi wa kuondoka kwenye kampuni iliyokuwa ikimsimamia.
Alieleza kuwa uamuzi huo haukuwapendeza baadhi ya wasimamizi wake. MB Dogg alidai kuwa maadui wake kwenye muziki walitoa pesa na kuzuia ngoma zake kuchezwa kwenye vyombo vya habari.
Soma Pia: Diamond, Zuchu na Nandy Wabwagwa Kwenye Tuzo za AFRIMA
Japo alipigana na mwishowe akapata heshima tena kwenye muziki, masaibu hayo yaliathiri nyota yake mno.
"Unayopitia konde mimi nilishapitia kuanzia miaka ya 2007 mpaka hivi sasa 2021...Nilipoamua kuondoka kwenye kampuni abdul alinipa baraka lakini hakuwa na furaha sikuelewa sababu ni nini hasa.Lakini nilianza kujua baada va kutoa ngoma yangu ya kwanza mwaka 2009 inayoitwa natamani.Pesa zilitoka kuzuia hii nyimbo isichezwe media zote na kipindi hicho hakuna digital platforms yeyote hapa bongo," sehemu ya chapisho la MB Dogg lilisomeka.
Leave your comment