Ibraah Azungumzia Utata Uliotokea Konde Music Worldwide Kabla ya ‘Jipinde’ Kuachiwa

[Picha: Kiss 100]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Konde Music Worldwide Ibraah ameelezea utata uliotokea katika lebo hiyo kabla ya ngoma yake iliyopewa jina la ‘Jipinde’ kutoka.

‘Jipinde’ iliandikisha historia kama ngoma ya Ibraah ambayo ilipata watazamaji wengi sana ndani ya muda mfupi. Kufikia sasa, ngoma hiyo imetazamwa takriban mara milioni tatu nukta nane kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Ibraah Atangaza ujio wa Albamu yake Mpya

Ibraah katika mahojiano aliyoyafanya kwenye kituo cha Efm alisimulia jinsi kulikua na utofauti wa kauli baina yake na usimamizi wa Konde Music katika kutoa ngoma hiyo.

Kwa mujibu wa Ibraah, yeye binafsi hakutaka ngoma hiyo itoke kwani hakuona kama ilikuwa imefikia kiwango cha ubora alichokitaka. Yeye alipendekeza ngoma tofauti itolewe ila meneja wake Jose Wamipango alisimama kidete na kusisitiza ‘Jipinde’ iachiwe.

Soma Pia: Ibraah Apendezwa na ‘High School’ Album ya Harmonize, Aitaja Albamu Bora Afrika

Meneja wake Ibraah alimshauri kuwa ‘Jipinde’ iachiwe kwa kipindi hicho alafu ngoma zingine ambazo alikuwa amependekeza yeye zikajumuishwe kwenye albamu yake.

Ibraah anatarajiwa kuachia albamu yake hivi karibuni baada ya bosi wake Harmonize kuachia albamu kwa jina la ‘High School’.

Kulingana na Ibraah albamu yake tayari ishakamilika. Alipoulizwa iwapo yeye na Harmonize kutoa albamu katika kipindi kimoja hakingeleta utata miongoni mwao, Ibraah alisema kuwa tayari alikuwa ashajadiliana na Harmonize kuhusu suala hilo na hakukuwa na tatizo lolote.

‘Jipinde’ ni moja kati ya nyimbo za Ibraah ambazo zimeandikisha mafaniko makubwa.

Leave your comment