Ibraah Atangaza ujio wa Albamu yake Mpya

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka huu wa 2021 umeonekana kuwa mwaka ambao wasanii wengi wamejitahidi kuachia albamu. Huku wasanii wakubwa wakigonga vichwa vya habari kutokana na albamu zao, msanii chipukizi Ibraah ametangaza kuwa yeye pia yuko mbioni katika kufanikisha albamu yake.

Ibraah alitoa tangazo hilo muda mfupi kabla ya bosi wake Harmonize kuachia albamu yake ya 'High School'.

Soma Pia: Ibraah Ajjibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Rayvanny

Kwa mujibu wa Ibraah, amewekeza muda mwingi sana katika kufanikisha albamu yake na ana matumaini makubwa kuwa mashabiki wake wataipokea vizuri.

Ibraah alikuua akizungumza wakati wa mahojiano na mwanahabari maarufu Millard Ayo. Taarifa hizi zimemfanya Ibraah kuwa gumzo sana miongoni mwa wadau mbali mbali kwenye tasnia ya muziki kwani anaonekana kuja kwa kasi mno.

''Taarifa ni za ukweli na tumuombe mwenyezi Mungu atupe uhai. Nina imani kitakuwa kitu kizuri kwa sababu nimespend a lot of time kwa hicho kitu. Nimekipa muda mwingi sana,'' Ibraah alieleza.

Taarifa hizi zilichipuka siku chache kabla ya Harmonize kuachia albamu yake ya pili iliyopwewa jina la 'High School'. Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo ishirini na imewahusisha watayarishaji wa muziki kumi na wawili.

Soma Pia: Ibraah Afichua Sababu ya Kumwacha Harmonize Marekani na Kurudi Tanzania

Albamu ya kwanza kutoka kwa Harmonize ilikuwa 'Afro East' ambayo iliachiwa mapema mwaka jana. Kwa upande mwingine, msanii nyota Alikiba anazidi kutamba kwenye anga za burudani kupitia albamu yake ya 'Only One King'.

Diamond Platnumz vile vile anasubiriwa kuachia albamu yake pia japo kufikia sasa hajadokeza lolote kuhusiana na albamu hiyo.

Leave your comment