Ibraah Ajibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Rayvanny

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Ibraah amefunguka kuhusu tetesi zinazoashiria uwepo wa uhasama baina yake na msanii kutoka lebo pinzani ya WCB Rayvanny.

Kwa muda mrefu tetesi zinazoashiria kuwa Ibraah hayuko katika hali ya mazungumzo na Rayvanny zimetawala mtandaoni.

Soma Pia: Ibraah Atangaza Tamasha Jipya ‘Ibraah Homecoming’

Tetesi hizi zilitokana na wimbo wa 'Hayakuhusu' aliouimba Ibraah. Kwenye ngoma hiyo, Ibraah alimkosoa vikali Rayvanny na kwa kiasi fulani akatumia maneno makali dhidi ya bosi huyo wa lebo ya Next Level Music.

Ibraah, hata hivyo, amesisitiza kuwa hakuna ugomvi baina yake na Rayvanny. Alieleza kuwa yeye yupo katika hali nzuri na Rayvanny na hawajakosana kwa lolote lile.

Akizungumzia ngoma yake ya 'Hayakuhusu', Ibraah alisema alitoa ngoma hiyo kama vile muziki wa kawaida na hakuwa na nia mbaya dhidi ya Rayvanny.

Soma Pia: Ibraah Afichua Sababu ya Kumwacha Harmonize Marekani na Kurudi Tanzania

Aliongezea kuwa hajutii kutoa ngoma hiyo. Kwa mujibu wa Ibraah, ameshawahi kukutana na Rayvanny na wakapiga stori.

“Siwezi kujuta na sitokuja kujuta kwa sababu nilichokifanya sio kitu kibaya. Tumekumbushana sisi ni vijana. Sisi sote tunajenga taifa moja. So unapomwona kijana mwenzio anateleza usikimbilie kumlaumu kwanza... So sina matatizo na mtu yeyote,'' Ibraah alisema.

''Nakumbuka nishawahi kukutana na yeye mara moja,'' Ibraah alijibu alipoulizwa iwapo ashawahi kukutana na Rayvanny.

Ibraah ni mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri sana kutoka lebo ya Konde Music Worldwide. Hivi maajuzi aliandamana na bosi wake Harmonize katika ziara ya muziki Marekani ambapo aliburidisha katika jukwaa kadhaa.

Leave your comment