Harmonize Atangaza Ziara Yake ya Muziki Nchini Kenya

[Picha: The New Times]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Harmonize ametangaza ziara yake ya muziki nchini Kenya. Ziara hiyo itadumu mwezi mzima wa Decemember huku tamasha lake la kwanza likifanyika tarehe nne mwezi huo katika mji wa Kakamega.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘High School’ Album

Harmonize alisema kuwa alipata msukumo wa kufanya ziara nchini Kenya kutokana na uungaji mkono mwingi ambao amekuwa akipata kutoka kwa wakenya.

Aliendelea kwa kusema kuwa analenga kuzuru angalau miji kumi mikubwa na kujaza viwanja vya matamasha yake. 'Teacher' kama anvyofahamika kiusanii, aliwaomba mashabiki wake ushauri katika kuchagua miji kumi ambayo atazuru.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Tofauti Iliokuwepo Katika Utengenezaji wa Albamu ya Afro East na High School

Kando na Kakamega, Harmonize bado hajafichwa jina la mji mwingine ambako ataburudisha.

''Full December in Kenya I can't wait. Mmekuwa mkinionyesha mapenzi kwa kiasi kikubwa sana tangu nilipo anza hii safari ya muziki nimechagua hii December kuja kuwalipa fadhira nitajitahidi kila niwezavyo atilist miji mikubwa (10) nifike this one will be stadium to stadium (4) stadium done tickets out next week oyaaa my first show will be 4/12/ (Kakamega),'' Harmonize alisema kwenye chapisho lake mtandaoni.

Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide alifichua kuwa atashirikiana na wasanii wa Kenya katika kutengeneza EP yake ijayo ambayo ataipa jina la 'Gengefleva'.

''But kwa sasa unachotakiwa kufanya nitajie mji ambao ungependa teacher asikose fika ...!!! Let's go we need (6) more stadiums. Kupitia hii tour nitahakikisha nashirikiana na wasani wenzangu wa Kenya kutengeneza (EP) ya ngoma 5 ambayo nitaiita (gengefleva) sitoangalia ukubwa wala udogo wa msanii lengo ni kuunganisha muziki wa Tanzania & Kenya so please nitajia msanii unaemkubali ambae unajua tukikutana kwenye ngoma kinawaka,'' Harmonize aliongezea.

Leave your comment