Alikiba Adokeza Ujio Wa Video Mpya Kutoka Kwa 'Only One King' Album

[Picha: Classic 105]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Alikiba amedokeza ujio wa video mpya kutoka kwenye albamu yake aliyoachia hivi maajuzi ya 'Only One King'.

Albamu hyo inazidi kufanya vizuri na kufikia sasa imepata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

Kutokana na ngoma hizo kufanya vizuri, Alikiba amepata msukumo wa kutoa video ya ngoma nyingine. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huy ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya King's Music aliomba mchango wa mashabiki wake katika kuamua ni ngoma gani atafanyia video.

"I'm thinking of Dropping the next Music video for a song from Only One King Album, tell me the visuals y'all want, type your choice on the comments!" ujumbe wa Alikiba ulisomeka.

Soma Pia: Producer Yogo Beats Asikitishwa Kuona Albamu ya Alikiba Ikiuzwa Mtaani

Katika chapisho lingine tofauti, Alikiba alifichua kuwa alifurahia sana walipokuwa wakirekodi video ya wimbo wa 'Oya Oya'. Aliongezea kuwa video hiyo ilirekodiwa nchini Afrika Kusini.

Wakati Alikiba anazidi kuteka anga za muziki kupitia albamu yake, mwenzake Harmonize ametangaza kuwa ataachia albamu yake mnamo tarehe tano mwezi ujao. Diamond Platnumz ambaye pia anatarajiwa kuachia albamu bado hajatangaza tarehe rasmi ya kuachia albamu hio.

Leave your comment