Rapa Moni Centrozone Amsifia Zuchu kwa Ustadi Wake wa Kuimba Nyimbo za Mapenzi

[Picha: Moni Centrozone Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mkali kutoka Tanzania Moni Cetrozone amejitokeza na kumsifu msanii nyota Zuchu kwa ustadi wake katika kutunga nyimbo za mapenzi.

Moni aliachapisha ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako pia aliambatanisha na video iliyomwonyesha akiuskiza wimbo wa Zuchu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Inatosha’, Nandy ‘Kunjani’ na Ngoma Zingine Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Kwa mujibu wa Moni Centrozone, amekuwa akiskiza nyimbo za Zuchu sana kwa siku za hivi karibuni na anapendia hisia ambazo anapata kutoka kwa nyimbo hizo. Aliongeza kwa kusema kuwa yeye kwa sasa amekua shabiki mpya wa Zuchu.

Moni alimmiminia Zuchu sifa kwa kusisitiza kuwa amependa kazi yake na ataendelea kusikiliza nyimbo za mapenzi.

"Oyaaaa Wahuni Nimenasa Sio Poa. Naenda Kama Shabiki Mpya. Nyie Huyu Dada Ana Balaa Sana Nimempenda. Wiki Hii Nzima Nasikiliza Ngoma Za Mapenz Tu Nna Mood," chapisho la Moni Centrozone mtandaoni ulisomeka.

Soma Pia: Rayvanny Ashukuru Mashabiki Kwa Mapokezi Mazuri Waliompa Mac Voice

Ujumbe wa Moni uliibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki huku wengi wakimuunga mkono kuhusu Zuchu kuwa na kipawa cha kuandika nyimbo nzuri.

Moni Centrozone pia alisifiwa kwa kumuunga mkono msanii mwezake na hivyo basi kuleta umoja katika tasnia ya muziki ya Tanzania.

Zuchu amesifiwa mno kutokana na mafanikio ambayo amepata ndani ya muda mfupi toka kutambulishwa kama mwanachama wa lebo ya WCB. Ndani ya takriban mwaka mmoja, tayari nyota ya Zuchu imeng'aa na kumpandisha ngazi katika muziki.

Leave your comment