Mac Voice Asimulia Alivyohangaika kufanya Muziki Hadi Karibu Ajitoe Maisha

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi kutoka Tanzania Mac Voice amefunguka kuhusu kisa ambacho kamwe hatowahisahau katika safari yake ya muziki.

Mac Voice akizungumza katika mahojiano na Wasafi FM alisema kuwa safari yake ya muziki hapo awali ilikumbwa na ugumu mwingi sana. Ugumu huu ulimsukuma Mac Voice kiasi cha yeye kukata tamaa na kutaka kujitoa uhai.

Soma Pia: Sababu Tano Kuu Zinazoeleza Mbona Tasnia ya Muziki ya Tanzania Inahitaji Tuzo Za Kinyumbani

Mac Voice hata hivyo anajutia kisa hicho kwani hakikua sahihi na anamshukuru Mungu kwa kumuepusha na kisa hicho.

"Unajua kwenye maisha tunahangaika sana, tunatafuta sana na pia inapotokea unatafuta sana na haujui muendelezo wako maishani inakuaje. Kidogo inakuaa ya kuumiza sana na pia inachanganya sana. Tukio ambalo siwezi kulisahau maishani mwangu ni kutaka kunywa sumu. Niweze kusema namshukuru mwenyezi Mungu kwa hatua ambayo alinipitisha kwa sababu nadhani pale ilikuwa ni hatua mbaya sana kwa sababu nilikuwa namkosea mwenyezi Mungu kwa kutaka kukatisha maisha yangu," Mac Voice alieleza.

Mac Voice amepata umaarufu baada ya kutambulishwa kama msanii wa kwanza chini ya lebo ya Next Level Music inayomilikiwa na mwanamuziki nyota Rayvanny.

Soma Pia: Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo

Tayari Mac Voice ashatoa EP yenye nyimbo sita ambazo zimepata mapokezi mazuri. Kabla ya kuingia Next Level, Mac Voice alikuwa akifanya muziki chini ya usimamizi wa msanii Chege.

Leave your comment