Rayvanny Na Iyanya Wadokeza Ujio Wa Ngoma Ya Pamoja

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Msanii Rayvanny ameendelea kutangaza jina lake kimataifa na hii ni baada ya msanii huyo kudokeza ujio wa ngoma mpya baina yake na msanii Iyanya kutoka Nigeria.

Collabo hiyo inakuja siku chache tangu wasanij hao wawili walipoonekana pamoja wakiwa nchini Ufaransa na pamoja na kutengeneza hamasa baina ya mashabiki kwamba huenda kuna collabo kati yao.

Rayvanny aliachia kionjo cha wimbo huo unaokwenda kwa jina la. "Zaza Zela" kupitia mtandao wa Tiktok ambapo tayari mashabiki mbalimbali wameanza kuufanyia challenge wimbo huo.

"Zaza Zela" umetayarishwa na Cee Beats na ngoma hiyo inatarajiwa kuwa collabo ya kwanza ya Rayvanny mwaka huu

Leave your comment