Nyimbo Mpya: Zuchu Ashirikishwa kwa ‘Upendo’ Ngoma Mpya ya Spice Diana [Video]

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Spice Diana kutoka Uganda amemshirikisha staa wa muziki kutoka WCB Zuchu katika wimbo wake mpya uliopewa jina la 'Upendo'.

Wimbo huu unasifia mapenzi yaliyonoga kwenye uhusiano. Mmoja baada ya mwingine wasanii hawa wawili wanasimulia jinsi wamezama kwenye mapenzi na raha wanayopata.

Soma Pia: Nandy Atangaza Tarehe ya Ziara Yake ya Muziki Marekani

Spice Diana anafungua wimbo huu na sauti yake nyororo na kuimba sehemu ya kwanza. "Umepata mabinti Lakini mimi napiga kama Kush Nimeshika maball Si wa Kampala wore nikawacrash. Jina langu ni Diana Nimekuana toka jana Sasa ka hatungekutana Kila kitu baby we are gonna do. Upendo, upendo upendo sio magic huu ni upendo Upendo, upendo Upendo sio magic huu ni upendo," Spice Diana anaimba.

Zuchu anaingia katika sehemu ya pili na kuongeza ladha kwa kuimba katika lugha ya Kiganda. Midundo ya ngoma hii imetayarishwa na Moko Genius chini ya usimamizi wa Source Management.

Soma Pia: Zuchu Alalamika Makampuni Kutowalipa Wasanii

Video ya wimbo huu ni ya hali ya juu na imezingatia mila ya kiafrika. Katika video hiyo, waliohusika humo ndani wanaonekana wakiwa wamevaa mavazi ya kiafrika.

'Upendo' umepokelewa vizuri na kufikia sasa umepata maelfu ya watazamaji. Licha ya ngoma hii kuwa ya Spice Diana, imechapishwa kwenye akaunti ya YouTube ya Zuchu ambayo iko na wafuasi zaidi ya milioni moja.

https://www.youtube.com/watch?v=n9oTjjfkXJA

Leave your comment