Mac Voice Aeleza Wosia Aliopewa na Diamond Kipindi Alijiunga na Next Level Music

[Picha: IPP Media]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Next Level Music Mac Voice amefunguka kuhusu wosia aliopewa na Diamond Platnumz kipindi anajiunga na lebo hiyo.

Mac Voice ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara akitembelea vyombo vya habari nchini Tanzania, ameeleza kuwa Diamond alikubali vilivyo kipaji chake na kumueleza kuwa ni muhimu kujituma, kuwa na nidhamu na subira.

Soma Pia: Mac Voice Afunguka Kuhusu Maisha Magumu Yaliyomsukuma Kufanya muziki

"Nakumbuka Diamond aliniambia una kipaji sana utafika mbali ila inabidi uzingatie vitu vitatu. Cha kwanza nidhamu, cha pili subira cha tatu kujituma. Huo ndio wosia alionipaga Diamond," alieleza mwanamuziki huyo.

Kwenye mahajiano hayo, Mac Voice pia alisema kuwa lebo ya Next Level Music inafanya kazi kwa ukaribu na WCB, kwa hivyo atakuwa akipokea mawaidha na wosia kutoka kwa wakuu wake kwenye lebo hizo mbili.

"Sisi wote ni familia moja. Next Level ni WCB, WCB ni Next Level. Support ni muhimu. Sawasawa mimi ni mjukuu wake (Diamond Platnumz) kwa hiyo kunisupport ni lazima. Lazima anisapoti," alizungumza Mac Voice.

Soma Pia: Sababu Nne Kuu Zinazowafanya Wasanii Wengi Tanzania Kuanzisha Lebo za Muziki

Kwa sasa, Mac Voice anatamba na EP yake ya My Voice yenye ngoma sita ambazo ameshirikisha wasanii wawili tu; Rayvanny na Leon Lee.

EP hio ilitumiwa kumtambulisha rasmi Mac Voice kama msani mpya wa lebo ya Next Level Music.

Leave your comment