Konde Music Worldwide Yatimiza Miaka Miwili Tangu Kuanzishwa

[Picha: East Africa TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki Harmonize anasherehekea miaka miwili tangu kuanzisha lebo yake ya Konde Music Worldwide.

Msanii huyo ambaye kwa sasa yupo Marekani kwenye ziara ya muziki, aliwashukuru mashabiki waliomuunga mkono tangu kutambulisho lebo hiyo.

Harmonize alifunguka kuwa lebo ya Konde Music Worldwide ilianza kama ndoto ambayo baadae iliwavutia watu wengi walioungana na yeye.

Soma Pia: Cheed Aeleza Chanzo Cha Ukimya Wake Tangu Ajiunge na Konde Gang

Miaka miwili baadaye, ndoto imepata mafanikio makubwa na kuwa moja ya lebo zinazoheshimika ndani na nje ya Tanzania. Harmonize, hata hivyo, alisema huu ndio mwanza na bado kuna mengi sana kutoka kwenye familia yake ya Konde Gang.

"Happy...!Happy! Anniversary. My dream team Konde Music Worldwide @kondegang I can't believe that we are (2) years Old Now it was Dream of Young Boy From Mtwara ...!!! Ikagusa Watu wengi I can't thank Everyone Enough But Trust Me this is Mwanzoo ...!!!! of So many things Silaha Yetu ni Watu na Watu Ni wewe Unaesoma Hapa ...!!! Now You Made Verry Big Team in The East Africa Siku Kama Ya Leo Ndio Niliitambulisha Rasmi @kondegang," Harmonize aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Wasifu wa Anjella, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mafanikio, Mahusiano na Thamani Yake

Meneja wa Harmonize ambaye anafahamika kama Mjerumani alidokeza kuwa kuna tangazo lipo njiani wakati wakiadhimisha miaka miwili ya Konde Music Worldwide.

"Tutasema jambo kuhusu anniversary ya konde music world wide mwaka huu anytime soon," ujumbe wa Mjerumani ulisomeka.

Leave your comment