Nyimbo Mpya: Barnaba Classic Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Mapenzi Yalaaniwe’

[Picha: Barnaba Classic Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Barnaba Classic ameachia ngoma mpya kwa jina 'Mapenzi Yalaaniwe'.

Ngoma hii inazungumzia machungu ambayo mhusika anapitia baada ya kupuuzwa na kutodhaminiwa na mpenzi wake.

Soma Pia: Diamond Aondoka Tanzania, Aelekea Marekani kwa Ziara Yake ya Muziki

Mhusika ambaye kwa nyimbo hii ni Barnaba Classic, anaelezea jinsi amejitolea kumpenda mwenziwe ila anahisi kwamba hapendwi kwa kiasi anachokitaka.

Mhusika amechoka kuteswa na moyo wake umejaa machungu na hivyo basi ameamua kulaani mapenzi, na hapo ndipo jina la 'Mapenzi Yalaaniwe' lilitokea.

"Don't waste my time Live your life if you don't love me. Mapenzi gani unani-stimulize Kutwa hupatikani kwenye line. Nikiuliza unapanick why? Why mpenzi Muda mwingine najiuliza why? Kivipi unanikosea Kama misamba nabinuka why? Ni wapi sijafikia," Barnaba anaimba katika sehemu ya wimbo huo.

Baranaba anazungumzia baadhi ya matatizo na matukio ambayo ameyapitia ndani ya uhusiano huo na yaliyomwacha na maumivu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia Video Mpya ‘Tamu’ Akimshirikisha Rayvanny

"Ashanilaza sana macho kodo Nikiamini atarudi on time Nikimuuliza uko wapi nafika mara moja Nimepita sehemu one time Nilijinyima kuvaa, nilijinyima na kale Ili mradi apencleze yeye to Nikajitenga na nclugu, nikamvumilia bubu Ili niwe na yeye to Nilikupa moyo wangu ila wapi? Wewe ukanilipa mengi makapi Nilikupa penzi ukanilipa chozi Yalaaniwe mapenzi," Barnaba anaimba katika kipande kingine.

Ngoma hiyo imetayarishwa ndani ya Kwetu Studios. Video ya ngoma hii inakwenda sambamba na mada yake.

Mandhari ambayo video ilirekodiwa pia yanapendeza. Wimbo huu umepokelewa vyema na ishapata maelfu ya watazamaji ndani ya muda mfupi.

https://www.youtube.com/watch?v=TfY89C5-68U

Leave your comment