Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia Video Mpya ‘Tamu’ Akimshirikisha Rayvanny

[Picha: Yinga]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hatimaye mwanamuziki Mac Voice ameachia video ya wimbo wake we ‘Tamu’ akimshirikisha rayvanny. Video hii ni ya pili kutokea kwenye EP yake ya ‘My Voice’.

‘Tamu’ ina mashairi matamu kama jina lake linavyojieleza. Mac Voice kwenye aya ya kwanza anatumia lugha ya picha kumsifia mwanamke ambaye anampenda akimfananisha na watu maarufu kama Tessy Chocolate na Jokate.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

"Sura Tessy chocolate kidoti Jokate katoto ni keki nitamwaga bajeti nikape tiketi kunipetipeti. Ulivyojazia ukinisisua utanizidia eeh nang'ang'ania nsije kuachia unanipatia eeh," anaimba Mac Voice.

Rayvanny anashika kijiti kwenye aya ya pili ya ngoma hii ya ‘Tamu’ ambayo imetayarishwa na Trone ambaye pia alihusika kutayarisha ngoma ya Zuchu ‘Sukari’.

Video ya ngoma hii inawaonesha Mac Voice na Rayvanny wakiwa wamezungukwa na wasichana warembo. Jinsi Mac Voice amejiachia na kutawala video hii ni ishara tosha kuwa kinda huyu yuko tayari kupeperusha vilivyo bendera ya Next Level Music.

Soma Pia: Nandy, Patoranking Waingia Studio Nchini Zanzibar

Kama ilivyokuwa kwenye ‘Nenda’, video ya ‘Tamu’ imeandaliwa na Eris Mzava ambaye amehusika kuandaa video nyingi za Rayvanny kama vile ‘Wanaweweseka’, ‘Sweet’ pamoja na ‘Siri’.

Kabla ya kuwa chini ya Next Level Music, Mac Voice alikuwa chini ya msanii Chegge.

https://www.youtube.com/watch?v=3mlDNZRkX6I

Leave your comment