Diamond Aondoka Tanzania, Aelekea Marekani kwa Ziara Yake ya Muziki

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Diamond Platnumz hatimaye ameondoka na kuelekea Marekani ambako ameratibiwa kuanza ziara yake ya muziki mnamo tarehe nane mwezi huu.

Tamasha la kwanza ambako Diamond atatumbuiza mashabiki wake ni katika mkoa wa Atlanta.

Soma Pia: Albamu 3 Zitakazosisimua Tasnia ya Muziki Tanzania

Baada ya kutumbuiza katika mkoa wa Atlanta, Diamond ataelekea Washingtone DC tarehe kumi, kisha baadae kutua katika mkoa wa Minneapolis tarehe kumi na tano.

Diamond atatumbuiza katika mikoa kumi na moja. Ziara yake itakamilika tarehe 31 mwezi huu.

Msanii huyo vile vile akiwa Marekani anatarajiwa kujihusisha na kazi ya kimuziki haswaa katika utengenezaji wa albamu yake. Albamu ya Diamond inaandaliwa nchini Marekani chini ya usimamizi wa mtayarishaji wa muziki Swizz Beats.

Albamu hiyo pia imewahusisha wadau wengine mbali mbali kutoka Marekani. Diamond aliagwa na wasanii kutoka lebo ya WCB ambayo anamiliki.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atuma Ujumbe kwa Mashabiki Kupitia Wimbo wa 'Kamwambie' 

Baadhi ya wasanii waliokuwepo akiondoka ni pamoja na Zuchu, Mbosso, Lavalava na wengine wengi. Aidha, kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond amewaanda mashabiki wake kwa tamasha lake la kwanza.

Aliwaarifu mashabiki wake kutokea kwa wingi. Wakati Diamond Platnumz anaondoka Tanzania ili kuanza ziara yake ya muziki, mwenzake Harmonize tayari anaendelea na ziara yake na ameshatumbuiza katika mikoa mbali mbali.

Wasanii hao wawili kuendeleza ziara zao za muziki kwa pamoja nchini Marekani kuna maana kuwa muziki wa bongo umekua na hadi kuwafikia wafuasi wake walioko nchi za kigeni.

 

Leave your comment