Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Ngoma Mpya ‘Mama’

[Picha: Premium]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya kuachia ngoma yake ya ‘Fofofo’ wiki kadhaa nyuma, mwanamuziki Aslay amerudi tena na bidhaa mpya sokoni ya kuitwa ‘Mama’.

Wengi tunamfahamu Aslay kwa uhodari wake wa kutunga nyimbo za mapenzi, lakini kwenye ‘Mama’, Aslay anabadilisha gia kwani wimbo huu ni makhususi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Cheed Aachia Ngoma 'Wandia'

Kwenye ngoma hii, Aslay anatumia dakika 3 na sekunde 46 kumsifia Rais wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoendelea kufanya tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka huu.

Aslay amemusihi Rais Samia kuendelea kufanya kazi ya kujenga nchi bila kuchoka.

"Mama kwa kweli unapambana kama ni kiu basi we ni maji twanenepeana. Mama tunakupenda sana umewapa nguvu na wawekezaji wanashindana mpaka. Najivunia kuzaliwa Tanzania, najivunia pia Rais wangu ni Samia mama kokotoa mama changanua hesabu za pwani na bara zote unazijua," anaimba Aslay.

Mtayarishaji wa ngoma hii ni Swahili Beats ambaye ameshafanya kazi nyingi na Aslay kama vile ‘Shangingi Mtoto’, ‘Vumilia’ na ‘Nashangaa’.

Ikumbukwe kuwa pia mwanamuziki Diamond Platnumz siku nne aliachia ngoma yake ya ‘Samia Suluhu’ ambayo pia ametoa sifa na pongezi nyingi kwa Rais Samia.

Wasanii wengine ambao wameshatoa ngoma za kumpongeza Rais Samia ni pamoja na Rapcha ‘Mtoto Wa Taifa’ pamoja na Zuchu kwenye ‘Kazi Iendelee’.

https://www.youtube.com/watch?v=ENNHwrQrDf0

Leave your comment