Nyimbo Mpya: Cheed Aachia Ngoma 'Wandia'

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka lebo ya Konde Gang Cheed ameachia ngoma yake ya kwanza chini ya lebo hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Wandia'.

Kwenye ‘Wandia’, Cheed anatumia sauti yake kama silaha ya kumsihi mpenzi wake anayeitwa ‘Wandia’ kumvumilia na kutunza pesa lao vizuri ili mambo yakikaa sawa waweze wote wawili kuishi vizuri.

Soma Pia: Harmonize Ahairisha Utambulisho wa Cheed Huku Rayvanny Akimpigia Mac Voice Kampeni

"Namiliki bodaboda penye nia pana njia Vidogo vimbogamboga najua unaumia vumilia tu. Vishilingi shilingi vibanie eeh come on Kopa kwa Mangi viunga robo tule" anaimba Cheed kwenye aya kwanza.

Ngoma hii imetayarishwa na mafundi wawili kutokea nchini Tanzania ambao ni Terriyo Monster kutokea Imagination Sounds na Mocco Genius ambaye ana wasifu wa kufanya kazi na wasanii wakubwa Tanzania ikiwemo Zuchu kwenye ‘Cheche’.

Soma Pia: Belle 9 Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na Wasafi, Konde Gang au Kings Music

Ikumbukwe kuwa Cheed alikuwa chini ya usimamizi wa Kings Music ambayo ni lebo ya Alikiba na ilipofika April mwaka jana, aliamua kung'atuka kwenye lebo hiyo.

Wiki iliyopita tarehe 24, Konde Gang ilikuwa imeandaa siku ya ‘Cheed Day’ ili kuachia ngoma hio, lakini sherehe iyo ilihairishwa.

Kulingana na Harmonize, ‘Cheed Day’ iliahirishwa kwa sababu zisizoweza kuepukika.

 "Siku zote mwenye subira bila shaka yupo karibu na Mungu. Najua kwa kiasi gani mnamsubiri Cheed ila ningependa kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba kwa sababu zilizopo kando ya uwezo wetu Cheed Day haitokuwepo tarehe 24/09/2021 kama tulivyopanga hapo awali. Tunawaahidi kuwajuzalini na siku gani hivi punde," chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

https://www.youtube.com/watch?v=Qz7IHha7JBI&feature=youtu.be

Leave your comment