Nyimbo Mpya: Maua Sama Aachia 'Zai'

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Maua Sama ameachia wimbo mpya kwa jina la 'Zai'.

‘Zai’ unazungumzia mwanamke ambaye amebaki na maumivu baada ya mume wake kumwacha na kuendea mwanamke mwingine ambaye anaitwa Zainabu, kwa kifupi Zai.

Soma Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Maua Sama kwenye wimbo huo anachukua uhusika wa mwanamke aliyempoteza bwanake na kupitia mistari anaeleza maumivu aliyonayo.

"Oya duku limekwama Hee nabado nampenda Ooya mwache Zai kwanza hey Au bado unampenda? What do you want me to do? Me I go die for you Sema lolote I go do Baby as long as I'm with you Zaiii zainabu wewe.. Ooh mume wangu me nampenda sand Zai Zai Zainabu wewe (You de break my heart oh break my heart) Zai Zainabu wewe (doh Zainab wewee) Zai Zai Zainabu wewe (You de break my heart breaks my heart) Why why ohh why why why You denying deny deny," Maua Sama anaimba katika sehemu ya ngoma hiyo.

Soma Pia: Maua Sama Adokeza Ujio wa Ngoma yake Rapa wa Marekani T Pain

Midundo ya ngoma hii imetayarishwa na na mtayarishaji wa miziki Mr. Simon.

Kwa sasa ngoma hiyo imetolewa kwa mfumo wa audio tu na video bado haijaachiwa. Maua Sama anatarajiwa kutoa video ya wimbo huo baadae.

Zai ni ngoma ya pili ambayo Maua Sama ameachia baada ya kuwa kimya kwa muda wa miezi saba. Maua alifichua hivi karibuni kuwa alikuwa kimya kwa sababu ya maradhi aliyokuwa akiugua ila kwa sasa amepona.

https://www.youtube.com/watch?v=6IE9ZGcvoeI

Leave your comment