Maua Sama Adokeza Ujio wa Ngoma yake Rapa wa Marekani T Pain

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Maua Sama ameonesha nuru mpya kwenye muziki wake baada ya kudokeza ujio wa collabo aliyofanya na rapa kutokea nchini Marekani T Pain.

Maua Sama alidokeza ujio wa collabo hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo ameonesha chats zake za Instagram na rapa T Pain huku kionjo cha ngoma hiyo kikisikika kwenye video hiyo fupi.

Soma Pia: Nandy Na Mr Eazi Waashiria Ujio Wa Kazi Yao Mpya

Maua Sama alitoa taarifa kuwa kesho mida ya saa mbili na nusu asubuhi ataachia ngoma kama ambavyo alifanya wiki iliyopita

"And its happening soon kesho (Friday) @ 8:30 AM muda wetu ni ule ule," aliandika msanii huyo.

Inakisiwa kuwa ngoma hiyo inayotarajiwa kuachiwa kesho ni remix ya ngoma yake ya ‘Away’ ambayo kwenye toleo la kwanza alimshirikisha Young Lunya.

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Lavalava, Mbosso Wamkaribisha Msanii Mpya Wa Rayvanny Mac Voice

T Pain ni moja kati ya marapa wenye heshima kubwa Marekani ambaye alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 2005 inayoitwa ‘Rappa Ternt Sanga’.

 Kufikia sasa, ameshatoa albamu sita za muziki huku akiwa ameshashinda tuzo mbili za Grammy mkononi na mpaka sasa ameshashirikiana kufanya collabo na wasanii kama Kanye West, DJ Khaled, Wiz Khalifa, Lil Wayne pamoja na Chris Brown.

 Ngoma ya ‘Away’ iliweza kufanya vizuri kwa muda mfupi tu tangu iingie sokoni kwani ilikuwa ni ngoma ya kwanza ya Maua Sama kwa takriban miezi sita. Mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube, ngoma hiyo ambayo bado haina video imeshatazamwa mara laki moja tisini na mbili.

Leave your comment