Nandy Na Mr Eazi Waashiria Ujio Wa Kazi Yao Mpya

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Huenda pakatokea EP mpya baina ya wasanii nyota Nandy kutokea Tanzania na Mr Eazi kutokea Nigeria iwapo mazungumzo yao kwenye mitandao ya kijamii ni ya kweli. Wanamuziki hao wawili ambao wako na ukaribu mno kimuziki, waliashiria ujio wa EP hiyo katika sehemu ya maoni ya chapisho la Nandy kwenye ukurasa wake wa Instagram. Nandy alikuwa amechapisha video iliyomwonyesha akiwa jukwaani akitumbuiza mashabiki. Mr Eazi kwenye sehemu ya maoni akamwomba Nandy watengeneze EP. 

Nandy bila ya kusita alimjibu Mr Eazi kwa kukubaliana naye kuwa watengeneze EP. Wasanii hao hata hivyo hawakuofichua habari zaidi kuhusiana na EP ambayo walikuwa wakizungumzia. Ikumbukwe kuwa ni muda mfupi tu baada ya Nandy kuachia EP yake ya Taste ambayo ilipokelewa vizuri sana na mashabiki. 

EP hiyo ilikuwa na ngoma nne ambazo ni Yuda, New Couple, Yote Sawa na Nimekuzoea. Kati hizo nyimbo nne iliyovuma sana ilikuwa 'Nimekuzoea'. Huenda ushirikiano baina ya Nandy na Mr Eazi ukatokana na makubaliano ambayo hao wawili walikuwa nayo hapo awali ambako Nandy alikubali kufanya kazi na kampuni ya Mr Eazi ya Empawa.

Nandy pia katika mahojiano ya hivi karibuni alieleza mbona amezingatia kutoa EP sana na wala si albamu. Kwa mujibu wa nyota huyo, albamu inatakiwa kazi mingi na pia kuwekeza muda. Kwa upande mwigine kutengeneza EP ni rahisi ikilinganishwa na albamu.

 

 

Leave your comment