Nay Wa Mitego Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mpya

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Nay Wa Mitego ameleta furaha kwa mashabiki wa muziki wake baada ya kutangaza kuwa yupo jikoni kuandaa albamu yake ambayo inategemewa kuingia sokoni.

Nay alitoa taarifa hizo kupitia akaunti yake ya Instagram upande wa Instastory ambapo msanii huyo alidokeza kuwa kufikia sasa maandalizi ya albamu hiyo yamefikia asilimia 50 na ngoma zote zinazofuata kutokea sasa zinaashiria ujio wa albamu hiyo.

Soma Pia: Meja Kunta Atangaza Ujio wa EP Yake Mpya

"Nipo tayari kuwaletea Album Heavy Album. Kuanzia Sasa Ngoma Zinazokuja Ni Ujio Wa Album. Mpaka sasa Ipo Asilimia 50%," aliandika msanii huyo kwenye Instastory.

Aidha, kwenye chapisho jingine Nay Wa Mitego alidokeza kuwa ataachia nyimbo siku 10 zijazo yaani tarehe 30 Septemba ikiwa zimeshatimia mwezi mmoja tangu aachie ngoma yake ya Rais wa kitaa.

Kwa sasa, Nay Wa Mitego anatamba na ngoma yake ya ‘Rais Wa Kitaa’ ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na wapenzi wa muziki kutokana na mashairi yake kugusa mambo mbalimbali ambayo yanatokea nchini Tanzania.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Albamu Mpya ‘Arizona’

Kufikia sasa, ‘Rais wa Kitaa’ imeshatazamwa takriban mara Milioni 1.4 kwenye mtandao wa YouTube.

Kwa mwaka huu, wasanii wa Hip-Hop kadhaa nchini Tanzania wameachia album kama vile Dogo Janja na Rapcha huku marapa wengine kama Rosa Ree, Stamina pamoja na Country Boy pia wametangaza kuja na albamu.

Leave your comment