Harmonize Atangaza Ujio wa Albamu Mpya ‘Arizona’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Gang Harmonize ameendelea kutoa habari njema kwa mashabiki wake baada ya kutangaza kuanza utengenezaji wa album yake mpya aliyoipa jina la ‘Arizona The Album’.

Soma Pia: Meja Kunta Atangaza Ujio wa EP Yake Mpya

Harmonize ambaye kwa sasa hupendelea kuitwa ‘Teacher’ ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti ya Instagram.

Nyota huyo amethibitisha hilo kwa kuchapisha video za mtayarishaji wa muziki anayeshirikiana nae kwa sasa Mr Simon ambaye ameeleza kuwa albamu hiyo itaitwa Arizona.

"Simon mtu mbaya yuko hapa tayari kwa ajili ya album inayofuata. Albamu yangu itaitwa Arizona kwa sababu nimetayarisha albamu hapa (Arizona)," alidokeza Harmonize.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Rayvanny, Jux, Marioo na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Taarifa hii ni mpya kabisa kutoka kwa Harmonize kwani kwa muda mrefu sasa amekuwa akidokeza na kutangaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa albamu yake ya ‘High School’ iko karibu kuachiwa.

Kwa sasa ‘Teacher’ yuko nchini Marekani na msanii mwenzie Ibraah kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ambayo inatarajiwa kurindima kwa takriban miezi mitatu nchini humo.

Kufikia sasa, ameshatumbuiza kwenye jimbo la Texas na wikiendi hii anatarajiwa kutumbuiza kwenye jimbo la Arizona.

Kwingineko, wasanii wote kutokea Konde Gang wametangaza kutoa albamu zao hivi karibuni kuanzia Killy, Ibraah, Country Boy na Anjella ambaye siku kadhaa nyuma alitangaza kutoa EP yake.

Leave your comment