Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Rayvanny, Jux, Marioo na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ni muda mwafaka sasa kwa wale wapenzi wa muziki kutokea nchini Tanzania kujumuika pamoja ili tuweze kuzipitia zile nyimbo kali ambazo zimepenya kwenye masikio ya wasikilizaji kwa wiki hii:

Soma Pia: Diamond ‘Naanzaje’, Jux ‘Sina Neno’, Harmonize ‘Teacher’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii 

Wanaweweseka – Rayvanny

Fundi wa muziki kutoka lebo ya WCB Rayvanny wiki hii alidondosha burudani ya kushiba kwa mashabiki zake kupitia ngoma yake mpya kabisa ya ‘Wanaweweseka’. Mdundo wenye ubunifu wa aina yake uliotayarishwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records pamoja na Sound Boy umefanya ngoma hii iwe bora sana.

https://www.youtube.com/watch?v=M6WisT8ocUE

Bia Tamu - Marioo

Baada ya kutetemesha taifa na ‘Mama Amina’ miezi kadhaa nyuma, Marioo ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Bia Tamu’. Ngoma hii ni makhususi kabisa kwa wale wapenda pombe na wapenzi wa kustarehe kwenye klabu za usiku pamoja na kumbi mbali mbali za starehe. Tangu wimbo huu utoke kuanzia redio mpaka kwenye mitandao ya kijamii watu wameupokea kwa mikono miwili.

https://www.youtube.com/watch?v=ACjpKIU973Y

Sawa - Balaa MC

Baada ya kutamba na ‘Nakuja Remix’, Balaa MC amezidi kuleta balaa zaidi kwenye muziki wa Singeli nchini Tanzania baada ya kuachia ‘Sawa’. Ngoma hii imetayarishwa na Eyo Kenny pamoja DJ Rider. Ubunifu wa kipekee umetumika na Balaa MC hasa kwenye kwenye ngoma hii .

https://www.youtube.com/watch?v=tXtnTg0DPm8

Sina Neno - Jux

Jux anaendelea kuonesha ubora wake kwenye utunzi wa nyimbo za taratibu na hii inadhirishwa na bidhaa yake mpya sokoni inayoitwa ‘Sina Neno’. Kwenye ‘Sina Neno’, Jux anampongeza mpenzi wake kwa kuingia kwenye mahusiano yake mapya na kupata ujauzito kitu ambacho mashabiki wengi wametafsiri kama ujumbe kwa mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee.

https://www.youtube.com/watch?v=QCtkOnnhOng

Lissa 2 - Rapcha

Kama kuna kitu ambacho Rapcha anakiweza kuliko wasanii wengine ni kuhadithia stori tena kwa uweledi uliotukuka na mkwaju wake mpya wa Lissa 2 unathibitisha usemi huo. Wimbo ambao huu ni muendelezo wa Lisa 1 umeweza kukosha sana mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=jVTOysre5Mo

Leave your comment