Rayvanny Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Next Level Music

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hayawi hayawi sasa yamekuwa kwani hatimaye Rayvanny siku ya leo amemtambulisha msanii wa kwanza anayeitwa Mac Voice kwenye lebo yake ya Next Level Music.

Rayvanny alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo alichapisha video fupi ya kumkaribisha msanii huyo kwa kuandika "Mtoto wa kwanza wa Next Level Music @macvoice_tz . Karibu kwenye familia kubwa. (First born @macvoice_tz welcome to the big family 24/9/2021)

Soma Pia: Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania

Mac Voice ndiye msanii wa kwanza kutambulishwa rasmi na Rayvanny tangu msanii huyo atangaze juu ya lebo yake ya Next Level Music miezi sita iliyopita.

Bila shaka, Rayvanny ametoa majibu kwa mashabiki ambao walikuwa wana hamu ya kujua nani amesainiwa kwenye lebo hiyo.

Kwa wafuatiliaji wa muziki nchini Tanzania, Mac Voice ni msanii ambaye kabla ya kusainiwa na Rayvanny alikuwa ameshatoa ngoma kadhaa huko nyuma na kuna kipindi alikuwa na ukaribu na msanii Chege na walitoa ngoma tofauti tofauti kama vile ‘Utarudi’, ‘Mama J’ na ‘Damu ya Ujana’.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

Baada ya ngoma hizo kufanya vizuri, Mac Voice alikaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo mpaka siku ya leo alivyotambulishwa rasmi kama msanii wa Rayvanny chini ya Next Level Music.

Kwa sasa, macho na masikio yapo hapo Next Level Music ili kujua Mac Voice ameaandaa kitu gani kwa mashabiki zake.

Leave your comment