Nyimbo Mpya: Maua Sama Aachia ‘Awa’ Akimshirikisha Young Lunya

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanumuziki wa Tanzania Maua Sama ameachia ngoma yake mpya yenye jina ‘Away’ ambayo amemshirikisha rapa Young Lunya.

‘Away’ ni wimbo wa mapenzi. Kwenye ngoma hii, Maua Sama anahadithia namna ambavyo anatamani kukutana na mpenzi wake baada ya kutoka safarini na anamuomba mpenzi wake ajiandae kumpokea pale atakapofika.

Soma Pia: Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki

Young Lunya hajawahi kufanya makosa pale anaposhirikishwa kwenye ngoma yoyote, na kwenye kibao hiki, anasikika zaidi kwenye ubeti wa pili ambapo nae pia anaelezea namna ambavyo anatamani kumuona mpenzi wake.

"Kusema ukweli naziwaza lips zako nimemiss kuzikiss mama mbalu na wewe ila sisikii drama. Naambiwa unacheat ila hizo habari habari siziskizi sana coz nakujua na nakuamini sana," anaimba Young Lunya.

Soma Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Kazi nzuri kutoka kwa mtayarishaji wa muziki kutokea Norway Mr Simon imefanya ngoma hii iwe ina hadhi ya nyota tano.

Ikumbukwe pia kwamba Mr Simon amehusika kutayarisha ngoma kama ‘All Night’ ya Anjella, ‘Mapenzi’ ya Ibraah pamoja na ‘Mama’ ya Young D.

‘Away’ ni ngoma ambayo imedhibitisha ujio mpya wa Maua Sama kwenye muziki baada ya kukaa takriban miezi sita bila kutoa ngoma yeyote kutokana na changamoto za kiafya.

https://www.youtube.com/watch?v=U6c6EyXcoAs

Leave your comment