Dully Sykes Adai Kuwa Miongoni mwa Waanzilishi wa Muziki wa Bongo

[Picha: Dully Sykes Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Dully Sykes amedai kuwa yeye ndiye muanzilishi wa muziki wa bongo. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Dully Sykes alisema kuwa yeye ni miongoni mwa wanamuziki wakongwe sana katika mtindo wa bongo.

Dully Sykes aliongeza kuwa alianza kuwa staa katika bongo miaka ya 1999 kabla ya wasanii wengi kujulikana. Sykes alijisifia kwa kuwa mmoja wa wasanii ambao waliutambua muziki wa bongo na kuufanya kuwa kitambulisho cha Tanzania kimuziki.

Soma Pia: Dully Sykes Akana Tuhuma za Ugomvi Baina Yake na Wasanii Wengine Bongo

Kwa sasa mtindo wa bongo umepata mafanikio makubwa na kutambulika sio tu Tanzania au barani Afrika tu bali duniani nzima.

"Mimi nimeanza kuwa staa nikiwa na miaka kumi na nane, mwaka wa 99, wangapi walikuwa wameshazaliwa? Unaona wachache sana," Dully Sykes alisema.

Dully Sykes alionyesha furaha na jinsi muziki wa bongo umekua na kusifia ujio wa mitandao ya kijamii ambayo imewasaidia wasanii wa kizazi kipya. Msanii huyo pia alisema kuwa kukua kwa muziki wa bongo kumewaongezea wanamuziki kipato.

"Siku izi vijana wamekuwa na nafasi kubwa kuliko sisi kwa sababu vijana wamekuta Facebook, vijana wamekutana Instagram, vijana wamekutana muziki wanapoenda kupiga show wanaikuta, zamani tukienda show Mbea, ina maana msanii ukisafiri unasafiri na muziki wako. Kwa hio kiukweli muziki kwanza umekua," Dully Sykes alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Biggie’

Kwa mujibu wa Dully Sykes, changamoto katika muziki zimepungua ikilinganishwa na hapo awali. Akitoa kauli yake kuhusu mtindo mpya wa Swahili Amapiano, Dully Sykes alisema kuwa haweziwalaumu wasanii wanaokwenda na mtindo unaovuma.

Alidai kuwa wanahabari katika tasnia ya burudani na vile vile ma DJ ndio wako na jukumu la kuhakikisha muziki wa bongo hautazimwa na mitindo mipya.

Leave your comment