Dully Sykes Akana Tuhuma za Ugomvi Baina Yake na Wasanii Wengine Bongo

[Picha: Dully Sykes Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka bongo Dully Sykes amekana madai kuwa kuna uhasama baina yake na wasanii wengine kutoka Tanzania.

Dully Sykes alikuwa akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni ambako pia alifunguka kuhusu suala la msanii mwenzake Harmonize kutumia mistari kutoka kwa wimbo wake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya ‘Wanaweweseka’

Dully Sykes ni mmoja wa wasanii wakongwe sana wa bongo flava na amekuwepo tangu enzi za zamani. Katika taaluma yake ya kimuziki, tuhuma zimeibuka kuwa ako na ugomvi na baadhi ya wasanii.

Mmoja wa wasanii ambao kwa siku za hivi karibuni amedaiwa kuwa na uhasama naye ni Harmonize. Hii ni kutokana na kuwa wasanii hao wawili ambao walikuwa marafiki wa karibu na hata kushirikiana kimuziki hawaonekani pamoja kama ilivyokuwa zamani.

Dully Sykes hata hivyo amesema kuwa hana ugomvi na Harmonize na bado ni marafiki. Katika mahojiano hayo hata hivyo Dully Sykes alidokeza kuwa huwenda kuna mgogoro wa kisheria kutokana na Harmonize kutumia mistari kutoka kwa wimbo wake.

Aidha alisisitiza kuwa wanasheria walimshauri kutolizungumzia suala hilo. Msanii huyo aliweka wazi kuwa hana ugomvi na msanii yeyote na kusema kuwa anawapenda wasanii wote bongo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Biggie’

 Dully Sykes hata hivyo alisema kuwa TID ndio msanii pekee ambaye ashawahi kuwa na uhasama naye. Aliongeza kuwa walisuluhisha tofauti zao na kwa sasa wao ni marafiki wa karibu.

"Ukaribu upo kwa sababu Harmonize ni mdogo wangu, kama wadongo wangu wengine. Kwa hiyo naweza nikafanya naye kazi siku yeyote na muda wowote kama wadungu zangu wengine. Alafu labda nikuambie kitu kingine, mimi sina tatizo na kijana yeyote," Dully Sykes alieleza.

Leave your comment