Nikki wa Pili Azungumzia Uwepo Wake Kwenye Muziki Licha ya Kupata Nafasi ya Uongozi

[Picha: Nikki wa Pili Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Nikki Wa Pili ambaye pia ni mwanachama wa Kundi la Weusi amedhibitisha kuwa ataendelea na muziki licha ya kuteuliwa kuwa DC wa wilaya ya Kisarawe.

Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Samia Suluhu alimteua Nikki Wa Pili kuwa DC, suala ambalo liliwapendeza wadau wengi katika tasnia ya muziki. Uteuzi huo pia uliibua maswali haswaa kuhusiana na uwepo wake kwenye Kundi La Weusi.

Soma Pia: Nikki wa Pili Aeleza Sababu Kuu Zinazoifanya EP Mpya ya Msanii Otuck Kuwa ya Kipekee

Akizungumza katika mahojiano na wanahabari, Nikki Wa Pili alisema kuwa yeye bado ni mwanamuziki na ataendelea kuwaburudisha mashabiki wake kupitia muziki. Nikki hata hivyo aliongeza kuwa shughuli za kikazi kama kiongozi huwa mingi na hivyo basi si muda wote atakuwa akihudhuria hafla za kimuziki.

Alisema kuwa atakuwepo katika nyimbo zitakazoachiwa na Kundi la Weusi hivi karibuni. Nikki pia alifichua kuwa atakua na miradi yake ya kimuziki na mashabiki wake watarajie kazi nzuri pia.

"Kiukweli ni ratiba, lakini kiongozi ni mtu pia unatakiwa uwe kwenye jamii na mimi ni msanii, mimi ni mwana entertainment. Nitaendelea kuwa balozi, nitaendelea kuwakilisha utamaduni wa burudani kwa hiyo pale ambapo nitakuwa na nafasi nitakuwepo, ukiona sijakuwepo basi nitakuwa tu nimekosa nafasi. Lakini mimi ni mwanaburudani na nitaendelea kuwa kwenye burudani," Nikki wa Pili alisema.

Soma Pia: Weusi Waeleza Jinsi Kundi Lao Litabadilika Baada ya Nikki wa Pili Kufanywa Mkuu wa Wilaya

Nikki wa Pili alikuwa akizungumza wakati alihudhuria uzinduzi wa EP ya msanii Otuck.

Leave your comment

Top stories

More News