Weusi Waeleza Jinsi Kundi Lao Litabadilika Baada ya Nikki wa Pili Kufanywa Mkuu wa Wilaya

[Picha: Weusi Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kundi La Weusi limesema kuwa itakuwa ngumu Nikki Wa Pili kuwa mshiriki hai wa kikundi hicho baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilya ya Kisarawe mkoani Pwani. Nikki Wa Pili, ambaye pia ni msemaji wa kikundi hicho, aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Jumamosi, Juni 19, 2021, kuongoza Kisarawe.

Soma Pia: Nikki wa Pili Kubaki na Kikundi cha Weusi Licha ya Kuapishwa Mkuu wa Wilaya

Nikki alichukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye alihamishiwa na kupelekwa Temeke, Dar es Salaam.

Joh Makini ambaye ni mwanachama wa kikundi hicho akizungumza hivi karibuni alisema kuwa Nikki Wa Pili atakuwa akichukua majukumu mengine rasmi kutoka kwa serikali na kwa hivyo itakuwa ngumu kwake kuendelea kutekeleza jukumu lake kwa kikundi.

Soma Pia: Moni Centrozone Ajiunga na Rooftop Entertainment

 Alibainisha kuwa wanamuunga mkono na watampa uhuru wa kuwatumikia watanzania katika nafasi yake mpya.

"Kuna vitu vitabadilika kwa sababu anaenda kulitumikia Taifa pale Kisarawe, hatuwezi kusema ataendelea kuwa msemaji wa Weusi kwa sababu anayohusika na nguvu kubwa ambayo tunamsapoti pia. Kwa hiyo kuweza kuona njia ya kufanya mambo mengine ambayo ilionekana kuwa huru zaidi kufanya kile kitu ambacho ameteuliwa kukifanya ambayo ni muhimu kwa sasa," Joh Makini alinukuliwa na The Citizen.

"Kiprotokol sidhani kama atakuwa anaruhusiwa kupanda kwenye jukwaa kwa sasa hivi. Kwa hivyo I think tunasubiri tuone jinsi mambo yatakavyo kuwa then tutafwata kitakachotakiwa kufutwa," mmoja wa Kundi la Weusi alisema.

Leave your comment