Nikki wa Pili Aeleza Sababu Kuu Zinazoifanya EP Mpya ya Msanii Otuck Kuwa ya Kipekee

[Picha: Otuck Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mnamo tarehe kumi mwezi huu msanii anayekuwa kwa kasi sana kutoka Tanzania Otuck aliachia EP yake iliyopewa jina la 'Future Memories'.

Soma Pia: Harmonize, Ibraah Wadokeza Ujio wa Kolabo ya Amapiano Baina Yao

Wasanii wakubwa pamoja na wadau wengine wa kuheshimika katika tasnia ya muziki ya Tanzania walihudhuria uzinduzi wa EP hiyo.

Miongoni mwa wasanii maarufu waliokuwepo ni pamoja na Jux, Ben Pol, Kundi la Weusi akiwemo Nikki Wa Pili pamoja na wengine wengi.

Nikki wa Pili ambaye ni mwanachama wa Kundi la Weusi na vile vile DC wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ni mmoja wa wasanii wanaojivunia uwezo mkubwa ikija katika masuala ya kimuziki.

Soma Pia: Anjella Ampongeza Country Wizzy Kwa Mafanikio Yake Kimuziki

Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo, Nikki wa Pili alieleza sababu zinazoifanya EP ya Otuck kuwa ya kipekee. Kwanza kabisa Nikki wa Pili alisema kuwa katika EP hiyo kuna nyimbo zilizotengenezwa kwa sababu ya soko tofauti.

Alisema kuwa mle ndani mna nyimbo zinazoeza kuchezwa katika mandhari tofauti na pia kulingana na hisia tofauti.

Aliongeza kuwa Otuck vile vile amejitambulisha kama msaniii mwenye uwezo mwingi kama mwanamuziki.

"EP kali, ipo kimuziki, ameonyesha talent, lakini ni EP ambayo unaweza ukasikiliza muda wowote iwe mchana. Kuna ngoma za kusikiliza usiku. Kwa hiyo nafikiri ameangalia audience tofauti, na ni EP ambayo unaweza uka play kwenye event tofauti. Kwa hivyo kimuziki hicho ndicho kitu cha msingi kwamba uwe na muziki ambao watu wakiwa kwenye sherehe wanaeza waka play, usiku anaeza akasikiliza, mchana anaeza akasikiliza na aka vibe nayo," Nikki wa Pili alisema.

Leave your comment

Top stories

More News