Harmonize, Ibraah Wadokeza Ujio wa Kolabo ya Amapiano Baina Yao

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutokea Tanzania Harmonize ameashiria ujio wa kolabo baina yake na msanii aliyemsaini kwenye lebo yake Ibraah.

Harmonize aliweka wazi uwepo wa kolabo hiyo kupitia Instagram Stories zake. Kulingana na chapisho za Harmonize, ngoma hiyo mpya itakuwa katika mfumo wa Amapiano.

Soma Pia: Ngoma ya Harmonize ya 'Fall In Love' Yachezwa BET

Ibraah kwa upande mwengine pia aliashiria kolabo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Msanii huyo hata hivyo hakusema mengi kuhusiana na ngoma hiyo, kando na kuchapisha picha ambazo zilimwonyesha akiwa na Harmonize studioni.

Wasanii hao wawili walionekana wakiwa katika mkutano na mtayarishaji wa muziki ambaye ni Mzungu.

Tangazo hilo kutoka kwa wasanii hao limechangamsha mashabiki wao kwani wasanii hao kila wakishirikiana hudondosha muziki mtamu.

Soma Pia: Harmonize Adai Muziki wa Kiafrika Utatawala Ulimwengu Mzima

Harmonize na Ibraah walishirikiana katika wimbo wa 'One Night Stand' ambao ulimpea Ibraah umaarufu mkubwa Afrika Mashariki. Kwa sasa Ibraah amekomaa kimuziki na hivyo basi katika kolabo hii pia ataweza kuwa na uzito wake kama msanii.

Ibraah kabla ya kuambatana na Harmonize kuelekea marekani aliachia wimbo wa 'Jipinde' ambao ulipata mapokezi mazuri.

'Jipinde' ilimuandikishia historia Ibraah kwa kupata watazamaji wengi sana ndani ya muda mfupi katika mtandao wa YouTube.

Wasanii hao wawili wako marekani kwa ajili ya ziara ya Harmonize ya kimuziki. Ziara hiyo inatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili.

Harmonize na Ibraah wataweza kuwatumbuiza mashabiki wao katika mikoa mbali mbali ya Marekani. Kwa sasa washatumbuiza katika baadhi ya mikoa hiyo.

Leave your comment

Top stories