Harmonize Adai Muziki wa Kiafrika Utatawala Ulimwengu Mzima

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Harmonize ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide amedai kuwa muziki wa kiafrika utateka ulimwengu mzima kwa siku za usoni.

Harmonize alitangaza kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Msanii huyo pia alichapisha video ambayo ipo kwenye albamu yake ya hivi karibuni iliyopewa jina la Afro East. Albamu hiyo kutoka kwa Harmonize imepata mapokezi mazuri miongoni mwa mashabiki na kufarahiwa sana.

Soma Pia: Ommy Dimpoz Adokeza Ujio wa Kolabo Yake na Nandy

Aidha, Harmonize pia alisema kuwa ana hamu sana ya kuitambulisha albamu yake ijayo. Mwanamuziki huyo hata hivyo hakufichua kiwango ambacho amefikia katika utayarishaji wa albamu yake ijayo.

"African music is now future of the world meet my sound #afroeast presenting East Africa sound... I can't wait to share my next album with you," chapisho la Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram ulisomeka.

Soma Pia: Nyimbo 5 zake Vanessa Mdee Zilizovuma Bongo

Kauli ya Harmonize inatokea muda mfupi baada ya wimbo wake wa 'Fall In Love' kuchezwa katika kituo cha runinga cha kimataifa cha BET.

Ngoma hiyo inapatikana katika albamu hiyo hiyo ya Afro East.

Harmonize kwa sasa yupo marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki inayotarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili.

Konde Boy kama anavyojulikana pia, atashiriki katika shughuli zingine za kimuziki akiwa huko Marekani. Ikija katika mjadala wa muziki wa Kiafrika kuteka ulimwengu, msanii mwengine ambaye itakuwa vigumu kupuuza jina lake kwenye mjadala huo ni Diamond Platnumz, ambaye hapo awali alikuwa marekani pia kwa shughuli za kimuziki.

Diamond vile vile alipata uteuzi katika tuzo za kimatifa za BET japo hakuweza kuibuka mshindi. Msanii mwenzake Burna Boy kutokea Nigeria alinyakua tuzo hiyo.

Leave your comment

Top stories