Wimbo ‘Busy Body’ wa Nuh Mziwanda Wafutwa YouTube

[Picha: Bongo 5]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Nuh Mziwanda kutokea Tanzania amepata pigo baada ya video yake ya ‘Busy Body’ kufutwa kwenye chaneli yake ya YouTube.

Nuh Mziwanda ambaye ni mojawapo ya wasanii wanaofanya vizuri sana Tanzania ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo msanii huyo ameonesha masikitiko yake kwa kuandika "Inauma Ila Nitazoea Busy Body haipo tena YouTube. God Bless You Rasta."

Soma Pia: Harmonize Adai Muziki wa Kiafrika Utatawala Ulimwengu Mzima

Bado haijafahamika ni sababu gani hasa iliyopelekea wimbo huo kufutwa YouTube na hata Nuh Mziwanda pia hajaelezea zaidi sababu ya video hiyo kufutwa kwenye mtandao huo.

Video ya ‘Busy Body’ iliachiwa mwanzoni mwa mwezi Agosti na ni wimbo ambao Nuh Mziwanda amemshirikisha rapa kutokea Konde Gang Country Wizzy huku audio ya wimbo hiyo imetayarishwa na S2kizzy ambaye amefanya kazi nzuri sana.

Read Also: Ommy Dimpoz Adokeza Ujio wa Kolabo Yake na Nandy

Changamoto kama hiyo pia imeshawahi kumkuta Harmonize kwenye wimbo wake wa ‘Uno’ kwani Novemba 2019 wimbo huo uliondolewa YouTube baada ya mtayarishaji muziki kutokea Kenya Magix Enga kudai kuwa Harmonize alitumia beat ya wimbo huo bila makubaliano.

Aidha, Ibraah kutokea Konde Gang wimbo wake wa ‘Wawa’ ambao amemshirikisha JoeBoy ulifutwa kwenye mtandao wa YouTube Mwezi Mei mwaka 2020 lakini kwa sasa unapatikana kwenye mtandao huo.

Leave your comment