Nandy Amsifia Rais Samia Suluhu Kwa Kukuza Sanaa ya Muziki Tanzania

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy amemsifia rais wa Jamhuri wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kukuuza sanaa ya muziki.

Katika chapisho aliloliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nandy alirejelea tukio ambalo rais Samia alimpigia simu wakati akitumbuiza katika tamasha lake la Nandy Festival.

Soma Pia: Nandy Atoa Shukrani Baada ya Tamasha lake Dar es Salaam Kupata Mafanikio Makubwa

Nandy alikiri kuwa alifurahishwa sana na kupewa motisha na simu hiyo kutoka kwa rais Samia.

Alieleza kuwa simu hiyo ni dhihirisho kuwa rais Samia yupo katika mstari wa mbele kwenye kukuza sanaa ya muziki nchini Tanzania. Nandy aliongeza kuwa rais Samia anawajali vijana nchini Tanzania.

"Moja kati ya mambo yaliyonipa nguvu kwenye #NandyFestival2021 ni simu niliyopokea kutoka kwa Rais @samia_suluhu_hassan. Simu ile ni udhibitisho kwamba #mamayukokazini kwa ajili yetu katika sekta ya sanaa na maeneo mengine yote," Nandy alisema.

Soma Pia: Diamond Aeleza Sababu ya kuachia Wimbo Wake Mpya 'Naanzaje'

"Rais wetu anayetujali sisi vijana na nchi kwa ujumla, anaendelea kuimarisha kila eneo na kuhakikisha tunakuwa na Tanzania tunayoitaka. Mimi nitaendelea kumuunga mkono, na kutimiza wajibu wangu, ili tuweze kusaidiana naye kujenga Taifa letu," Nandy aliongezea.

Aidha, Nandy sio msanii wa kwanza kupigiwa simu wakati akitumbuiza mubashara. Msanii tajika kutokea lebo ya WCB Zuchu pia alipigiwa simu wakati akitumbuiza katika tamasha lake la Zuchu Homecoming lililofanyika mkoani Zanzibar.

Rais Samia amesifiwa kwa kuishika mkono tasnia ya muziki nchini Tanzania. Hayati rais John Maghufuli pia alisifiwa kwa kuwashika mkono wasanii na kuleta umoja baina ya wasanii wenye uhasama nchini Tanzani.

Leave your comment