Darassa Atangaza Kuachia Wimbo wa Injili Hivi Karibuni

[Picha: Abby Chams Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa mtindo wa kufoka Darassa ametangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa wimbo wake ujao hivi karibuni utakuwa wimbo wa kumtukuza Mungu.

Kwenye taarifa aliyochapisha mtandaoni, Darassa alikiri kuwa safari yake ya muziki pamoja na mashabiki wake imekua ndefu mno, na sasa ilikuwa muda wa kubadili njia na kuanza safari nyingine tena.

Aliweka wazi kuwa ngoma yake ifuatayo imepewa jina la 'King Of The Kings' kwa maana ya 'Mfalme wa Wafalme'. Ngoma hiyo ameifanya Darassa kwa ushirikiano na Abby Chams.

Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

Kwaya ya injilisti ya Kijitonyama vile vile ilkuwa na mchango katika utayarishaji wa ngoma hiyo.

Mdundo wa wimbo huo umetayarishwa na Producer Abbah. Kwa sasa ngoma hiyo ingali jikoni ila Darassa amewapa mashabiki wake fursa ya kuweza kuiagiza kabla ya kutoka ili itakapotoka wale walioagiza watapata wa kwanza.

Rapa huyo pia alifichua kuwa asilimia sabini ya kipato kitachotakana na wimbo huo kitatumika kuwasaidia mayatima.

"Wakati hawa vijana wanatoka kuja kucheza hapa! Wacha watu wazima tufanye mambo ya maana. Leo ninayo furaha kuwatangazia tulianza na nyinyi kama utani, Na tumetokea gizani but LookatUsNowCMG we’re officially company," Darassa alisema.

Soma Pia: Zuchu Adhibitisha Uwepo wa Kolabo Nyingine Baina Yake na Rayvanny

"Mauzo au mapato kutoka digital platforms na chanzo chochote cha kuingiza pesa kupitia wimbo huu 70% zitakwenda kusaidia kwenye vituo vya watoto wenye uhitaji (Orphanages).Hii ni program endelevu lengo ni kusaidia kujenga jamii zetu au kuboresha, Kusaidia watoto watoke mitaani ili tusipoteze nguvu ya kujenga We’re CMG kwenye MUNGU tuna aminia Kwenye Kazi tunapigania," rapa huyo aliongezea.

Leave your comment