Frida Amani Athibitisha Kufanya Kazi na Rosa Ree

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwana Hip-hop mashuhuri nchini Tanzania Frida Amani hatimaye amejitokeza na kuthibitisha kuwa wimbo wa pamoja kati yake, Rosa Ree na Chemical uko jikoni.

Kwa muda mrefu, ujio wa wimbo ambao utawahusisha wasanii hao watatu imekuwa ni kitu kilichovutia sana mashabiki hasa baada ya wasanii hao kuonekana pamoja studio siku ya Jumapili.

Soma Pia: Rosa Ree, Frida Amani na Chemical Waingia Studio Kutengeza Wimbo wa Pamoja

Frida Amani ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Imo’ aliomshirikisha Mimi Mars kupitia mahojiano yake aliyofanya kwenye kipindi cha The Switch amethibitisha ujio wa wimbo huo na kudokeza kuwa wazo la wasanii hao kuja pamoja lilianza kwa msanii Rosa Ree.

"Idea ya kukutana kwa pamoja ilitoka kwa Rosa Ree kwa sababu anayo album ambayo inakaribia kutoka so kwenye albamu yake ametamani kuwa na sisi. Na its a great energy nadhani ni kitu kizuri,” alisema Frida.

Soma Pia: Rosa Ree Atangaza Kukamilisha Albamu Yake

Aidha Frida Amani aliongeza kuwa wimbo huo kwake yeye utakuwa ni wa pili kufanya akiwa na rapa Rosa Ree.

"Kwangu mimi hii ni mara ya pili kukutana nae ( Rosa Ree) kwenye ngoma moja times zimebadilika targets are different so ni kitu kizuri," alidokeza msanii huyo.

Kwa sasa, wanahabari, wadau wa muziki na mashabiki wako macho sana kusubiria wimbo huu ambao bila shaka unatarajiwa kuwepo kwenye albamu ya Rosa Ree inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Leave your comment