Beka Flavour Akubaliana na Wazo la Kuirudisha Yamoto Band Pamoja

[Picha: Beka Flavour Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Beka Flavour ambaye ni mwanachama wa zamani wa bendi ya Yamoto amekubaliana na wazo la kulirudisha kundi hilo pamoja kwa sababu ya mashabiki na pia kibiashara. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni na Wasafi FM, Beka Flavour alieleza kuwa muziki kwa sasa ni biashara na hivyo basi panapotokea nafasi ya kutengeneza hela basi wadau husika wanapaswa kuketi chini na kuona jinsi wazo hilo litatekelezwa.

Soma Pia: Beka Flavour Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mpya

Msanii huyo akijadiliana na mwanahabari wa Wasafi FM alikubali kuwa kulirudisha kundi hilo pamoja, japo kwa tamasha moja tu, kutawavutia mashabiki wengi sana na kuwafanya wao kama wasanii kufaidika.

"Watu wakifanya mipango sidhani kama itashindikana. Ata Mkubwa (Fella) mwenyewe akifanya...Si biashara tu," Beka Flavour alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Beka Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘In Love’ na ‘Umerogwa’

Kundi la Yamoto Band lililokuwa na wanachama wanne ambao ni; Beka Flavour, Aslay, Marombosso (Ambaye kwa sasa anafahamika kama Mbosso) na Beka Flavour, lilivuma sana enzi yake huku likiwa chini ya usimamizi wa Mkubwa Fella.

Kundi hilo lilijulikana si kwa ngoma zao za kupendeza tu bali kwa mbwembwe na burudani haswaa wakiwa jukwaani. Kwa bahati mbaya, tofauti ziliibuka baina ya wanachama wa Yamoto Band na kuelekea kuvunjika kwake.

Kila msanii alienda zake na kuwa mwanamuziki huru. Kuna waliopata mafanikio makubwa wakiwa huru ila wengine wao walididimia kidogo ikilinganishwa na ushawishi waliokuwa nao kama Yamoto Band. Hata hivyo, hamna mwanachama mwengine wa kundi hilo ambaye ameongelelea suala la kuunganisha kundi hilo.

Leave your comment

Top stories

More News