Nyimbo Mpya: Beka Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘In Love’ na ‘Umerogwa’

[Picha: Beka Flavour | Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa bongo Beka Flavour ameachia nyimbo mbili mpya 'In Love' na ‘Umerogwa'.

Kwenye wimbo wa 'In Love', Beka Flavour anachukua uhusika wa mtu ambaye yuko kwenye mapenzi na anasifu uhusiano wake. Anaelezea jinsi anavyompenda mpenzi wake na kuongeza kuwa haogopi kuonyesha ulimwengu kuwa yuko katika mahusiano na yeye.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Mdundo wa wimbo huu umetayarishwa na Mafia akishirikiana na Mr. T Touch. Mdundo huo ni wa kasi ya chini ili kusaidia katika kutimiza maudhui na hali ya mapenzi.

"Najinenepea sasa kidonge, mahaba unayonipa kwa nini nikonde, walahi wacha wanidonge, tunavyopendana hatuna mawenge . Penzi unalonipa la kisultan, kuna muda nahisi niko peponi," Beka Flovour aliimba.

https://www.youtube.com/watch?v=DDyA1kR5DPM

Katika wimbo wa pili wa ‘Umerogwa’, Beka Flavour anabadilisha mada na kukosoa vikundi anuwai vya watu katika jamii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

Wimbo huu ulitayarishwa na Jaco Beats na Gachi B. Mdundo ni wa kasi kidogo na unakaribiana midundo ya Afrika Kusini ya Amapiano.

Ni muhimu kuashiria kuwa wanamuziki mbali mbali kutoka Bongo wametengeneza nyimbo kwa kutumia midundo ya Amapiano na hii inaonekana kuwa mwenendo mpya.

Kwa sasa, video za nyimbo hizi mbili bado hazijaachiwa, lakini zintarajiwa kutoka hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=6Cl1m_inKBo

Leave your comment

Top stories

More News