Beka Flavour Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mpya

[Picha: Pinterest]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote, msanii Beka Flavour ametangaza rasmi ujio wa albamu yake ambayo itakuwa ya kwanza tangu aanze muziki. Akifanya mahojiano kwenye kituo cha Times Fm, Beka Flavour alisema kuwa  maandalizi ya albamu yake ndio kitu kilichomfanya kuwa kimya kwa muda mrefu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Beka Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘In Love’ na ‘Umerogwa’

"Watu walikuwa wanalalamika kwanini hutoi nyimbo, ilikuwa niko busy naandaa albamu na albamu hio alhamdudilahi imeisha na itakuwa na nyimbo 14," Beka Flavour alinena.

 Beka Flavour hakuishia hapo aliweka wazi pia kuwa kwenye albamu hiyo atashirikisha wasanii wa ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo wasanii kutokea nchi kama Kenya, Nigeria na Rwanda.

"Nimefanya kazi na wasanii tofauti tofauti lakini siwezi kuwataja saizi nadhani albamu ikitoka watu wataona nimefanya na watu kutoka Nigeria, watu kutoka Kenya yaani sehemu tofauti kwa hiyo albamu ikitoka watu watafahamu nimefanya na nani na nani," alisema msanii huyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

Kwenye mahojiano hayo, Beka Flavour pia aliweka wazi kwanini aliwachia nyimbo mbili; ‘In Love’ pamoja na ‘Umerogwa’ kwa mpigo.  "Ni kama zawadi ambayo nimejizawadia, kwa hiyo mimi nimejizawadia nyimbo mbili lakini pia zawadi kwa mashabiki zangu ambao wanasupport muziki wangu."

Kando na Beka Flavour, wasanii wengine kutokea nchini Tanzania kama Young Lunya, Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize na Marioo wametangaza kutoa albamu mwaka huu.

Beka Flavour alianza kujulikana kwenye tasnia ya muziki mwaka 2013 kwenye kundi la ‘Yamoto Band’ na ilipofika mwaka 2017 kundi hilo lilivunjika na tokea hapo ameshatengeneza nyimbo nyingi kama ‘Kibenten’, ‘Sikinai’, ‘Libebe’ na ‘Naona Kiza’.

Leave your comment

Top stories

More News