Nyimbo Mpya: Quick Rocka Aachia EP Yake ‘Love Life’

[Picha: Quick Rocka Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarafu kutoka Bongo Quick Rocka ameachia EP yake mpya yenye jina ‘Love Life’.

Quick Rocka ambaye ukiachana na kuimba pia ni mtayarishaji muziki, mfanya biashara na muigizaji ameachia EP hiyo iliyosheheni nyimbo nne ambazo ni ‘Love Song’, ‘Te Amo’, ‘Ukimya’ na ‘Kabinti’.

EP hii imetayarishwa na watu wanne ambao ni Amy Waves, Bob Manecky, Tuphy pamoja na Quick Rocka mwenyewe huku maandalizi ya mwisho yakishughulikwa na nguli wa muziki Chizan Brain.

Soma Pia: Baba Levo Agoma Kuachia EP, Atoa Masharti kwa Mashabiki Wake

Kimaudhui EP hii ya Love Life kama jina linavyojitanabaisha inahusu mapenzi na visa vyake kama kufurahi, kuachwa pamoja na changamoto zilizi kwenye mahusiano.

Kwenye EP hii, Quick Rocka hakutaka kushirikisha msanii yeyote bali aliimba nyimbo zote mwenyewe. Akielezea kwanini ameamua kufanya EP nzima peke yake bila kushirikisha msanii mwingine yoyote, Quick Rocca alisema kuwa "Hii acha iende tu mi mwenyewe imekuwa kitambo kidogo sijaachia nyimbo nilizoimba mi mwenyewe nimekuwa nikishirikisha shirikisha watu, let me do this four songs Quick Rocka mwenyewe then zitazofuata zitakuwa ni collabo."

 Aidha Rocka aliweka wazi kuwa EP hii ni matunda ya yeye kukaa kimya muda mrefu na huu ni mwanzo tu, kwani baada ya muda anategemea kuachia albamu yake ambayo ameipa jina la ‘Life of Baba’ ambayo hajaeleza itatoka lini na ni wasanii gani watashirikishwa.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Huu ni ujio mpya wa Quick Rocka kwenye muziki kwani alikaa kimya muda sasa na alikuwa kujikita sana kwenye kuandaa muziki pamoja na kuigiza kwenye tamthiliya mbalimbali.

Leave your comment