Baba Levo Agoma Kuachia EP, Atoa Masharti kwa Mashabiki Wake

   

[Picha: Baba Levo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Baba Levo ametangaza kuwa hataachia EP yake aliyopanga kuitoa hivi karibuni mpaka pale atakapofikisha wafuasi laki moja kwenye akaunti yake ya YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Baba Levo alichapisha picha yenye maneno yaliyosomeka " Sitoi EP yangu mpaka nifikishe subscribers 100k".

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Ujumbe huu kutoka kwa Baba Levo unakuja siku chache baada ya kutangazia umma kuwa anatarajia kuachia EP hivi karibuni iliyosheheni nyimbo tano na zote zitakuwa na midundo ya kuchangamka au "amsha popo".

Aidha, siku mbili zilizopita, Baba Levo aliweka wazi kuwa wasanii wawili wakubwa ambao ni Diamond Platnumz pamoja na The African Princess Nandy wamekubali kushirikishwa kwenye EP hiyo japo hakuweka bayana kuwa itakuwa kwenye wimbo mmoja ama kila mtu atakuwa kwenye wimbo wake.

Mara baada ya kutoa taarifa hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram. watu wengi walionekana kuitikia wito kwani saa moja baadae alichapisha picha inayoonesha kuwa wafuasi wameongezeka na kufikia sasa wamefikia wafuasi themanini na tisa elfu kwenye akaunti yake ya YouTube.

Soma Pia: Zuchu Asimulia Alivyokaribia Kuacha Muziki Akiwa WCB

Hii si mara ya kwanza kwa msanii kutokea Tanzania kugoma kuachia kazi mpya kisa YouTube Moni Centrozone tarehe Juni 15 aliweka wazi kuwa hataachia albamu mpaka pale akaunti yake ya YouTube itakapofikisha wafuasi laki moja.

Baba Levo ni mmoja ya watu maarufu sana nchini Tanzania. Kando na muziki mzuri anaoufanya na kazi yake ya Utangazaji pale Wasafi, Baba Levo anasifika kwa kipaji cha kuchekesha ambacho kimemfanya awe na wafuasi wengi.                    

Leave your comment