Ney wa Mitego Azungumzia Madai Kuwa ana Ugomvi na Harmonize

[Picha: All Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Hip-hop kutokea Tanzania Ney wa Mitego kwa mara ya kwanza amefichua chanzo cha yeye kutokuwa na maelewano mazuri na msanii mwenzake Harmonize.

Ni vema kukumbuka kuwa siku chache zilizopita, akiwa kwenye mahojiano na kituo cha EATV Ney aliweka wazi kuwa Harmonize ‘amemblock’ kwenye mtandao wa Instagram bila ya yeye kufahamu chanzo.

Soma Pia: Babalevo, Kajala Wajikosha Kwa Wimbo wa Harmonize huku Mwijaku Arukia 'Iyo' ya Diamond

Katika mahojiano mengine aliyoyafanya kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa Clouds FM, Ney alisema kuwa yeye binafsi hana ugomvi na Harmonize.

"Mimi sina tofauti na Harmonize nadhani labda yeye tu atakuwa amecatch tu kawaida lakini mimi sina tatizo nae," alisema Ney.

Aidha Ney alizidi kudokeza kuwa anahisi tatizo lilianza pale alipoombwa na Harmonize kushiriki wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Bedroom remix’, amabapo alidai kuwa Harmonize hakumwambia ukweli kuhusu wasanii gani watashiriki kwenye wimbo huo.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Wenye Jina ‘Mang'dakiwe’ Remix Wiki Hii

"Kwanza alinidanganya wimbo wa Bedroom remix aliniambia kuna wasanii watatu tu ama wanne alimtaja Darassa, Khaligraph na yeye lakini baadae baada ya kujua nikappreciate tu sawa mwanangu mimi nafanya vocal nikamtumia," Ney alidokeza.

Ney alidai kuwa hata baada ya kumtumia Harmonize kipande chake alichorekodi, Harmonize alichelewa kumuarifu siku ya kwenda kurekodi video.

"Baada ya kumtumia baadae siku mbili tatu yani akanipigia simu kwamba eeh bwana tunashoot, okay nikamwambia tunashoot? tunashoot lini? Leo jioni. Brother kweli kabisa tunaenda vitu kienyeji hivyo mi nina shughuli za kufanya, inawezekana mimi ni muziki huo huo usinipeleke kama sina ratiba nyingine," alieleza msanii huyo.

Video ya ‘Bedroom remix’ ilitoka tarehe 9 Aprili mwaka 2020 na Harmonize kwenye wimbo alishirikisha wasanii wa Hip-hop pekee. Wasanii waliohusika kwenye wimbo huu ni Darassa, Country Wizzy, Rosa Ree, Billnass, Badhdad, Young Lunya pamoja na Moni Centrozone kutoka Rooftop Entertainment.

Kufikia sasa video ya ‘Bedroom Remix’ imetazamwa mara ilioni tatu nukta nane kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment