Babalevo, Kajala Wajikosha Kwa Wimbo wa Harmonize huku Mwijaku Arukia 'Iyo' ya Diamond
3 August 2021
[Picha: The Citizen]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Waswahili wanasema siku zote sikio halikatai muziki mzuri na bila shaka Mwijaku pamoja na Baba Levo wamethibitisha usemi huu baada ya kuonekana wakicheza nyimbo za wasanii ambao mara nyingi huonekana wakiwakosoa.
Video aliyoichapisha msanii Diamond Platnumz kwenye akaunti yake ya Instagram inamuonesha Mwijaku ambaye mara kadhaa humkosoa Diamond Platnumz kwenye masuala tofauti tofauti akicheza wimbo wa ‘Iyo’ uliotoka hivi karibuni.
Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Wenye Jina ‘Mang'dakiwe’ Remix Wiki Hii
Mwijaku ambaye ni mtangazaji wa redio hapa nchini anakumbukwa kwa kukosoa Rolls Royce ya Diamond Platnumz aidha alikuwa ni miongoni mwa watanzania wachache walioonyesha furaha baada ya Diamond kukosa tuzo ya BET.
Tazama Video HAPA
Kwa upande mwingine, Baba Levo ambaye ni mfuasi mkubwa wa Diamond Platnumz na mkosoaji mkubwa wa Harmonize ameonekana dhahiri shahiri akicheza wimbo wa Harmonize ‘Anajikosha’ pamoja na ‘Sandakalawe’ akiwa na muigizaji Kajala Masanja ambaye ni mpenzi wa zamani wa Harmonize.
Soma Pia: Nyimbo Mpya:Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo na Rayvanny, Marioo na Barakah the Prince
Ni muhimu kukazia pia Baba Levo amekuwa ni hasimu mkubwa wa msanii Harmonize mathalani alimkosoa msanii huyo baada ya Harmonize kumnunulia msanii wake Anjella gari. Kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram watu wengi wameonekana kushtushwa na video hizo na baadhi ya watu kusema kuwa hiyo ni dalili kuwa hakuna uhasama kati ya pande hizo mbili.
Tazama Video HAPA
Mwijaku ni nani?
Mwijaku ni mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena kinchorushwa Clouds Fm kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa. Akiwa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mwijaku alipata umaarufu 2014 baada ya uwepo wake kwenye tamthiliya inayoitwa ‘Mahusiano’ iliyokuwa inaruka Clouds Tv. Baada ya tamthiliya hiyo kumalizika ndipo aliingia rasmi kwenye utangazaji na amepata umaarufu maradufu baada ya mara kwa mara, kumkosoa vikali Diamond Platnumz kwenye vyombo vya habari.
Baba Levo ni nani?
Baba Levo ni mwanamuziki mkongwe mzuri na pia aliwahi kuwa diwani wa Mwanga Kaskazini kupitia chama cha ACT Wazalendo. Kwa sasa ni mtangazaji pale Wasafi kwenye kipindi cha Mgahawa.
Leave your comment