Otile Brown Ahairisha Kolabo yake na Darassa

[Picha: Otile Brown Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kolabo iliyotarajiwa kwa hamu sana baina ya mwanamuziki wa Kenya Otile Brown na mwenzake kutoka Tanzania Darassa imeharishwa hadi wiki ijayo.

Hapo awali, Otile Brown alikuwa ametangaza kuwa ataachia wimbo kwa ushirikiano na Darassa. Katika ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Otile Brown alisema kuwa walikuwa wamepanga kuachia video hiyo tarehe 30 mwezi Julai ila ilibidi wahairishe kwa sababu zisizoepukika.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Damian Soul Aachia EP Mpya ‘Mapopo’

Otile Brown alieleza kuwa mipango ya kuachia wimbo wake haikuwa imekamilika na tayari wiki ilikuwa mwishoni. Hata hivyo aliahidi kuwa ngoma hiyo itadondoshwa wiki iijayo japo hakutaja siku kamili.

"Nafahamu tulistahili kuachia wimbo wiki hii ila kuna mambo hayajakaa sawa … na kwakua wiki tayari imeisha … tunaomba tutoe wiki ijayo," Ujumbe wa Otile Brown katika mtandao wa Instagram ulisoma.

Mashabiki wengi walikuwa wamesubiria haswaa kumsikiza Darassa na jinsi mtindo wake wa kufoka ungeingiana na mtindo wa Otile Brown wa kuimba nyimbo za mahaba. Darassa amekuwa vutio kubwa kwa wasanii wa Kenya. Wiki chache tu zilizopita, alishirikishwa na msanii Jovial kutoka Kenya katika wimbo wa ‘Usiku Mmoja’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

Ngoma hiyo ilipokelewa vyema na mashabiki na kwa sasa imefikisha takriban watazamaji nusu milioni katika mtandao wa YouTube.

Leave your comment