Jinsi Diamond, Alikiba Walivyomtumbuiza Malcom Ally Aliyeuguwa Zaidi ya Miaka Kumi

[Picha: The Star]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtangazaji maarufu kutokea Tanzania kwa jina la Masoud Kipanya anaomboleza kifo cha mwanawe Malcom Ally aliyefariki mnamo tarehe 28 mwezi Julai akiwa Dar es Salaam.

Malcom Ally alifariki baada ya kuugua kuwa muda wa zaidi ya miaka kumi. Malcom Ally wakati akiigua alipendwa sana na wengi huku watanzania kwa wakati huo wakimwombea apone.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

Ripoti zinaonyesha kuwa Malcom hakupata masiha ya kawaida kwani alikuwa kitandani siku zote na hakuweza kucheza na wenzake wale kuenda shule. Malcom Ally alipendwa na wasanii wengi wa bongo ambao walimtembelea nyumbani kwao na kumtumbuiza wakati akiwa kitandani.

Wanamuziki wa Tanzania walimwombea apate nafuu na kumtia moyo kila wakati walimtembelea. Miongoni mwa wasanii wakubwa ambao walimtembelea na kumtumbuiza Malcom Ally ni pamoja na Diamond na Alikiba.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny, Marioo, Alikiba na Wasanii Wanaotarajiwa Kuachia Wimbo Mpya Wiki Hii

Malcom alikuwa karibu sana na wasanii hawa wawili. Alikiba alimtambua Malcom kama rafiki wake mkubwa sana. Wakati Diamond alienda kumtembelea Malcom, aliandamana na timu yake nzima.

Sehemu aliyokuwa Malcom nyumbani kwao ilikuwa imefurika na watu waliopendezwa na jinsi Diamond alivyokuwa amekuja kumtakia heri Malcom. Aidha, Diamond aliimba nyimbo kadhaa akiwa kando yake Malcom huku akionekana mwenye furaha sana.

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Amapiano Zilizoachiwa na Wasanii Kutoka Bongo

Mara kwa mara wakati akitumbuiza alimpa Malcom kipaza sauti kusudi yeye pia aimbe naye.

Alikiba kwa upande wake hakuambatana na watu wengi. Katika video iliyorekodiwa, Alikiba alionekana akiimba pamoja na Malcom wimbo wake wa zamani wa Cinderella. Malcom alisikika akiimba pamoja na alikiba na alikuwa amezishika mistari za wimbo huo.

Alikiba kupitia ukurasa wake wa Twitter aliomboleza kifo cha Malcom Ally. "Inna Lillahy Waina Illahy Rajioun. Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha rafiki yangu Malcom Ally Masoud, mtoto wa kaka yangu @masoudkipanya - Allah amuweke mahala pema peponi. Malcom, awape uvumilivu na imani familia yake," Alikiba aliandika mtandaoni.

Mamake Diamond Platnumz pia alituma rambirambi zake kupitia mtandao wa Instagram.

Leave your comment