Nyimbo Mpya: Barakah The Prince Aachia ‘Rainey’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kutokea nchini Tanzania, Mwamba anayesifika kwa sauti nzuri Barakah The Prince ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Rainey’.

‘Rainey’ unamzungumzia mwanaume anayempenda binti lakini binti tayari yuko kwenye mahusiano na mtu mwingine hivyo basi Barakah anamsihi binti huyo kuwa iwapo mahusiano yake yatavunjika, yeye yuko tayari kumpokea.

Soma Pia: Barakah The Prince Adai Wimbo Wake ‘Yanachosha’ Ndio Ngoma Mpya Bora Zaidi Bongo

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu Barakah anaimba: "Mpaka lini utalalamika wewe kuwa anakutesa yeye na wakati mi hisia zangu nilishakuonesha na hata hujali wewe."

Barakah anaendelea kutiririsha mashairi kwa binti huyu akiimba "Kwako maumivu ukichoka kwangu nafasi ipo. Huku shamba la mapenzi tosha, utavuna upendo siku ukihisi amekuchosha beba mpaka virago. Kwako mlango wazi kwako nahitaji pendo lako."

Wimbo huu umetayarishwa na nguli wa muziki kutokea nchini Tanzania Dedley ambaye pia amehusika kutayarisha wimbo mpya wa Chidi Benz unaoitwa King of the Jungle."

Soma Pia: Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

Huu ni wimbo wa pili kutoka kwake mwaka huu kwani Juni 10 aliweza kuachia wimbo wa ‘Yanachosha’ ulioweza kufanya vizuri kwenye chati mbali za muziki hapa nchini Tanzania.

Aidha,mara tu baada ya kuachia wimbo huu Barakah alitambulisha kwa mara ya kwanza kampuni ya Skyfye ambayo yenyewe itahusika kusimamia kazi zake nje ya Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Barakah alindika: "Kwa wapenzi wa muziki wangu na mashabiki zangu kwa ujumla leo ninayo furaha kubwa kutambulisha kwenu skyefye music kama company itakayosimamia project zangu kimataifa kwa maana ya nje ya mipaka ya Tanzania"

Wimbo wa ‘Rainey’ bado haujafanyiwa video na ndio wimbo wa kwanza wa Barakah The Prince tangu atie wino na kampuni ya Skyfye.

https://www.youtube.com/watch?v=Hg3iPfLXG-o

Leave your comment